Matokeo ya Azam vs KMKM Leo 24/10/2025

Matokeo ya Azam vs KMKM Leo 24/10/2025

LEO, Azam FC watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam, wakiwakaribisha KMKM kutoka Zanzibar kwenye mchezo wa marudiano wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup).

Mchezo huu unatarajiwa kuanza saa 11:00 jioni na utarushwa mubashara kupitia Azam Sports 2 HD. Azam FC inaingia kwenye pambano hili ikiwa na faida ya mabao mawili waliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa visiwani Zanzibar.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Oktoba 18, 2025, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Azam FC walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM. Mabao hayo yalifungwa na Jephte Kitambala Bola dakika ya 6, huku Pascal Msindo akihitimisha bao la pili dakika ya 42.

Matokeo hayo yanaipa Azam FC nafasi nzuri kuelekea mchezo wa leo, kwani inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kusonga mbele katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Kwa upande mwingine, KMKM inakabiliwa na kazi ngumu ya kusaka ushindi wa mabao 3-0 ili iweze kutinga hatua ya makundi. Hata hivyo, historia inaonesha kuwa hakuna kati ya timu hizi mbili ambayo imewahi kufika hatua hiyo katika michuano ya kimataifa tangu zilipoanzishwa.

Matokeo ya Azam vs KMKM Leo 21/10/2025

Matokeo ya Azam vs KMKM Leo 24/10/2025

Azam Fc VS Azam Fc

Historia na Rekodi za Azam FC katika Michuano ya CAF

Timu ya Azam FC, inayojulikana kwa jina la “Wanalambalamba”, imekuwa miongoni mwa klabu za Tanzania zinazowakilisha nchi katika mashindano ya CAF kwa miaka kadhaa. Rekodi yao kubwa ilikuwa mwaka 2013, walipofika raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika na kutolewa na FAR Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 2-1.

Safari ya Azam FC msimu huu imekuwa ya kuvutia. Katika raundi za awali, waliishinda El Nasir ya Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 8-1, kisha wakaitoa Barrack Young Controller II ya Liberia kwa mabao 2-1. Matokeo haya yameonesha ukuaji wa kiwango cha timu hiyo na kuongeza matumaini ya kuandika historia mpya msimu huu ikiwa watafanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga SC Yatangaza Kuachana na Kocha Wake Romain Folz
  2. Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026
  3. Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  4. Pacome Anukia Kombe la Dunia Baada ya Ushindi 7-0 Dhidi ya Shelisheli
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo