Matokeo ya Coastal Union vs Yanga Leo 07/12/2025

Matokeo ya Coastal Union vs Yanga Leo 07/12/2025

Wagosi wa Kaya Coastal Union leo wanashuka dimbani kuutafuta ushindi muhimu dhidi ya mabingwa watetezi Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu NBC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kuanzia saa 1:15 usiku.

Huu ni mpambano ambao unatarajiwa kuvuta hisia kubwa kwa kuwa pande zote mbili zinaingia zikiwa na malengo makubwa, huku rekodi zao za karibuni zikiibua maswali mengi kuhusu hatma ya pointi tatu muhimu.

Coastal Union inaingia kwenye mechi hii ikiwa chini ya kocha Mohamed Muya, ikijikuta katika kipindi kigumu cha rekodi mbaya inapokutana na Yanga. Tangu mwaka 2022, Wagosi wamepasuka mara nane mfululizo mbele ya Wanajangwani, huku ushindi wao wa mwisho ukiwa Machi 4, 2021 walipowalaza Yanga kwa bao 1–0.

Kwa ujumla, timu hizi zimekutana mara 24 katika Ligi Kuu Bara tangu 2011. Coastal imeshinda mara tatu, Yanga ikibeba ushindi mara 16, huku michezo mitano ikimalizika kwa sare.

Kwa msimu huu, mwenendo unaendelea kuwa na sura tofauti: Coastal imeshinda mechi moja, kutoka sare tatu na kupoteza moja katika michezo mitano iliyopita. Yanga, kwa upande mwingine, imeshinda mechi nne na kutoa sare moja bila kupoteza mchezo wowote.

Uwanja wa Jamhuri umegeuka makazi ya muda ya Coastal kufuatia kufungiwa kwa Uwanja wa Mkwakwani – hali iliyowakosesha mashabiki wa Tanga nafasi ya kuiona timu yao ikipambana na Yanga kwa takribani misimu miwili. Hata hivyo, Jamhuri nao haukuwa mkombozi sana msimu huu, kwani Wagosi wameambulia pointi moja pekee katika michezo miwili waliyocheza hapo.

Coastal Union: “Wanapigika… zamu yao kulia”

Kauli mbiu ya Coastal kwa mchezo wa leo “Wanapigika… zamu yao kulia” inaakisi shauku ya kikosi hicho kutaka kukomesha uteja uliodumu kwa miaka minne mfululizo. Timu hiyo inajivunia wachezaji kama Maabad Maulid, Athuman Masumbuko na nahodha Bakar Msimu, ambao wote wanatarajiwa kuwa chachu ya kuvunja ngome ya Yanga inayoongozwa na Djigui Diarra, Dickson Job na Bakar Mwamnyeto.

Kocha Muya, ambaye pia alishawahi kukutana na Yanga na kupoteza akiwa na Fountain Gate, alisema kuwa heshima kwa wapinzani haitaondoa dhamira ya kupata matokeo:

“Naheshimu sana ubora wa Yanga… mechi ya leo tumejipanga kufanya vizuri, Mungu akileta kheri wachezaji wakiamka vizuri na wafuate maelekezo niliyowapa basi mashabiki wa Coastal Union watafurahi,” alisema.

Nahodha Bakar Msimu aliongeza akisema:

“Uwanja wa Jamhuri umetupa pointi moja katika michezo miwili tuliyocheza hapa msimu huu… tumejipanga vizuri kupata pointi tatu.”

Yanga SC: Ubora, Mwendokasi na Rekodi ya Kutopoteza

Kwa upande wa Yanga, mchezo huu ni sehemu ya mkakati wa kuendelea kudhihirisha ubora wa kikosi chao ambacho hakijapoteza takriban mechi 25 mfululizo. Mara ya mwisho Wanajangwani kukinikwa walipoteza 3–1 mbele ya Tabora United (sasa TRA United) mnamo Novemba 7, 2024.

Kocha Pedro Gonçalves anaendelea kuwategemea wachezaji wake nyota kama Pacome Zouzoua, Prince Dube, Maxi Nzengeli na Duke Abuya. Akiuelezea mchezo wa leo, Pedro alisema:

“Namba za wapinzani wetu hazidanganyi… kila mara tukikutana nao tunakuwa na mchezo mgumu. Tunajua hautakuwa mrahisi lakini tuna kikosi bora na tutapambana kuhakikisha tunaondoka na pointi tatu.”

Akizungumzia maandalizi ya muda mfupi, aliongeza:

“Maandalizi yetu siyo makubwa kwa sababu ya muda mchache kutoka mchezo uliopita… lakini kwenye akili zetu tunajua ni nini tunataka na tuko hapa kutafuta ushindi.”

Mchezaji Offen Chikola alizungumzia motisha ya wachezaji kabla ya mchezo:

“Tumejiandaa vizuri kuwakabili Coastal Union… tunajua umuhimu wa mchezo wa leo na tumejipanga kuondoka na ushindi.”

Matokeo ya Coastal Union vs Yanga Leo 07/12/2025

Matokeo ya Coastal Union vs Yanga Leo 07/12/2025 (LIVE UPDATE)

Coastal Union VS Yanga Sc

Hiki Apa Kikosi cha Yanga Vs Coastal Union Leo 07/12/2025

Taarifa Za Mchezo

🏆 #nbcpremierleague
🆚 Coastal Union
🗓️ 07 December 2025
🏟️ Jamhuri, Dodoma
⏱️ 01:15 Usiku

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  2. Matokeo ya Simba vs Azam Leo 07/12/2025
  3. Coastal Union vs Yanga Leo 07/12/2025 Saa Ngapi?
  4. Kikosi cha Simba vs Azam Leo 07/12/2025
  5. Simba vs Azam Leo 07/12/2025 Saa Ngapi?
  6. Ratiba ya Mechi za Leo 07/12/2025 Ligi Kuu ya NBC
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo