Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)

necta matokeo kidato cha nne

Haya Apa Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2024/2025, maarufu kama “Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025.” Matokeo haya ni muhimu sana kwa sababu huamua mwelekeo wa elimu ya wanafunzi kwa ngazi za juu kama Kidato cha Tano au vyuo vya kati.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na NECTA, jumla ya watahiniwa 477,262 kati ya wanafunzi 516,695 waliofanya mtihani wamefaulu kwa kupata madaraja ya I, II, III, na IV. Hii ina maana kwamba asilimia 92.37 ya watahiniwa wamefaulu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3 ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 89.36.

Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya I, II, na III imeongezeka hadi kufikia 221,953, sawa na asilimia 43. Hii ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo watahiniwa 197,426, sawa na asilimia 37.4, walipata madaraja hayo. Kwa upande mwingine, idadi ya watahiniwa waliopata daraja la IV na zero imepungua, jambo ambalo limepelekea ubora wa ufaulu kupanda kwa asilimia 5.6.

Katika mgawanyo wa kijinsia, kati ya watahiniwa 477,262 waliofaulu mtihani wa Kidato cha Nne, wasichana ni 249,078 sawa na asilimia 52, huku wavulana wakiwa 228,184, sawa na asilimia 48. Hata hivyo, kwa kuzingatia ubora wa ufaulu wa madaraja ya I hadi III, wavulana wamefanya vizuri zaidi kwa asilimia 54 (119,869) ikilinganishwa na wasichana ambao ni asilimia 46 (102,084).

NECTA imebainisha kuwa matokeo haya yanaonesha juhudi kubwa zilizofanywa na wanafunzi, walimu, wazazi, na wadau wa elimu katika kuboresha viwango vya elimu nchini Tanzania. Wasichana wamefaulu kwa wingi zaidi, lakini wavulana wameonyesha ubora mkubwa wa ufaulu kwa madaraja ya juu. Hii inaashiria umuhimu wa kuendeleza juhudi za kuboresha elimu kwa jinsia zote.

Kwa kuzingatia umuhimu wa matokeo haya, NECTA imesisitiza kuwa ni vyema kwa wanafunzi waliopata matokeo mazuri kuchangamkia nafasi za kujiunga na Kidato cha Tano au vyuo vya kati, huku wale waliokutana na changamoto wakishauriwa kuchukua hatua madhubuti za kurekebisha mapungufu yao na kuendelea na safari ya elimu.

Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)

Angalia Matokeo ya Kidato cha Nne Kupitia Viungo hapa chini

ALL CENTRES
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi A
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi B
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi C
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi D
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi E
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi F
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi G
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi H
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi I
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi J
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi K
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi L
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi M
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi N
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi O
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi P
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi Q
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi R
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi S
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi T
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi U
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi V
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi W
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi X
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi Y
Matokeo ya Shule Zinazoanza na herufi Z

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)
  2. NECTA: Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 (Form Four Results)
  3. Ratiba Ya Mtihani Wa NECTA Kidato Cha Sita 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo