Matokeo ya Pamba Jiji vs Yanga Leo 08/04/2026
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo wanashuka dimbani kuendeleza kampeni yao ya kutetea ubingwa kwa mchezo mgumu dhidi ya Pamba Jiji utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uimara wa Pamba Jiji wanapocheza nyumbani msimu huu.
Muhtasari wa Mchezo
Katika pambano hili la leo, Yanga wanaingia wakiwa vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara, wakiongoza kwa tofauti ya pointi sita. Ushindi dhidi ya Pamba Jiji utaongeza pengo hilo na kuwapa nafasi nzuri zaidi ya kujitanua kileleni dhidi ya wapinzani wao wakuu.
Kwa upande wa Pamba Jiji, timu hiyo imeonyesha ubora mkubwa nyumbani ambapo haijapoteza mechi yoyote msimu huu. Rekodi hiyo inajumuisha sare mbili muhimu dhidi ya Azam (2-2) na Simba (1-1), jambo linaloifanya kuwa timu ngumu kwa wageni.
Kikosi cha Yanga: Habari Muhimu Kabla ya Mchezo
Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na hali nzuri ya kujiamini baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons, ushindi uliokuja baada ya sare tatu mfululizo zilizoweka presha kwa mabingwa hao.
Hata hivyo, kikosi hicho kitaendelea kumkosa kipa wao namba moja, Djigui Diarra, anayekitumikia adhabu ya kukosa mechi tatu. Licha ya hilo, mlinda mlango Aboutwalib Mshery ameendelea kung’ara akiwa hajaruhusu bao lolote msimu huu.
Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni uwezekano wa kurejea kwa washambuliaji wao wawili hatari, Prince Dube na Laurindo Aurelio ‘Depu’, ambao wote wanaongoza kwa ufungaji ndani ya kikosi hicho wakiwa na mabao sita kila mmoja.
Kikosi cha Pamba Jiji na Tishio lao
Pamba Jiji wataingia uwanjani wakitegemea zaidi safu yao ya ushambuliaji ikiongozwa na Mathew Tegis, ambaye ndiye kinara wa mabao kikosini akiwa na manne, pamoja na Peter Lwasa mwenye mabao matatu.
Kwa mujibu wa kocha wao Francis Baraza, timu hiyo ina wachezaji wenye uzoefu mkubwa ndani ya ligi, jambo ambalo linawapa imani ya kupata matokeo chanya:
“Ukiangalia kwenye ligi timu yetu ina wachezaji wazoefu wanaoijua Ligi ya Tanzania, najivunia sana ubora wao… naamini tunakwenda kupata matokeo mazuri,” alisema Baraza.
Rekodi na Historia ya Mikutano
Historia inaipa Yanga faida kubwa katika mechi hizi. Tangu Pamba Jiji irejee Ligi Kuu, haijawahi kuifunga Yanga, ikipoteza michezo yote mitatu iliyopita kwa jumla ya mabao 10-0.
Msimu huu, timu hizo zilipokutana duru la kwanza, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0. Pia msimu uliopita katika Uwanja wa CCM Kirumba, Pamba Jiji ilifungwa 3-0 kabla ya kupoteza tena 4-0 ugenini.
Fuatilia Hapa Matokeo ya Yanga vs Pamba Jiji Leo 08/04/2026
| Pamba Jiji | Vs | Yanga Sc |
Kauli ya Kocha wa Yanga
Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, alikiri ugumu wa mchezo huo lakini akaonyesha imani kwa kikosi chake:
“Tunakwenda kukutana na timu nzuri ambayo imekuwa ikifanya vizuri sana ikiwa nyumbani, lakini tuna timu nzuri ambayo tunataka kuendelea kushinda kwenye michezo yetu.”
Takwimu Muhimu za Yanga
- Haijapoteza mechi yoyote msimu huu
- Imefunga mabao 35
- Imeruhusu mabao matatu pekee
- Inaongoza msimamo wa ligi kwa pointi sita mbele
Mapendekezo ya Mhariri:
- Droo ya Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza: Man City Yapangwa na Southampton, Chelsea Uso kwa Uso Dhidi ya Leeds
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali FA Cup Pemba
- Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 06/04/2026
- Simba SC Yashindwa Kuambulia Pointi Mbele ya Azam FC Dabi ya Mzizima
- Ratiba ya Ligi Kuu NBC Leo 04/04/2026








Leave a Reply