Matokeo ya Simba vs Gaborone Leo 28/09/2025
Wekundu wa Msimbazi Simba SC wapo dimbani leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, wakikamilisha mechi ya marudiano dhidi ya Gaborone United ya Botswana katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huu, ambao ni muhimu kwa mustakabali wa klabu hiyo msimu huu, umepangwa kuanza saa 10:00 jioni.
Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 walioupata ugenini Francistown, Botswana, wiki iliyopita. Matokeo hayo yanaipa nafasi ya kusonga mbele kwa sare ya aina yoyote au ushindi wa nyumbani.
Hata hivyo, kama Gaborone United watashinda kwa tofauti ya mabao mawili au zaidi, Simba itaondoshwa kwenye mashindano, hali inayoongeza presha na umakini kwa kikosi cha Msimbazi.
Matokeo ya Simba vs Gaborone Leo 28/09/2025
Simba SC | vs | Gaborone |
Historia na Tahadhari kwa Simba
Mashabiki wa Simba hawajasahau machungu ya msimu wa 2021/2022, ambapo baada ya kushinda ugenini kwa mabao 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy, timu ilipoteza mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam kwa mabao 3-1 na kuaga mapema mashindano. Historia hiyo ni funzo muhimu kwa klabu, ikionyesha kwamba matokeo ya ugenini pekee hayatoshi bila umakini wa marudiano.
Kauli za Makocha Kabla ya Mechi
Kocha Mkuu wa Muda wa Simba, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amewatoa hofu mashabiki wake akisisitiza kwamba kikosi chake kimejiandaa ipasavyo.
“Sijawahi kupoteza kwenye mechi ya kwanza ya mashindano na naamini wachezaji wangu wako tayari kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na kufuzu. Tunaomba mashabiki waendelee kutuombea,” alisema Morocco.
Kwa upande mwingine, Kocha wa Gaborone United, Khalid Niyonzima, ameweka wazi kwamba timu yake haioni presha licha ya kupoteza mchezo wa kwanza.
“Bao moja halimaanishi tumeshindwa. Tunafahamu Simba ni timu kubwa lakini na sisi tupo tayari kupambana. Mashabiki wetu wasubiri furaha baada ya mchezo huu,” alisema Niyonzima.
Matarajio ya Mechi na Hatua Inayofuata
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani mkali kutokana na hali ya matokeo ya awali. Mshindi wa jumla kati ya Simba na Gaborone United atakutana na mshindi kati ya Simba Bhora ya Zimbabwe na Nsingizini Hotspurs ya Eswatini katika raundi inayofuata.
Kwa upande wa klabu nyingine ya Tanzania, Azam FC, itashuka dimbani saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuikabili El Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini. Azam ina nafasi nzuri baada ya kushinda mabao 2-0 ugenini, ikihitaji sare au hata kupoteza kwa tofauti ya bao moja ili kufuzu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba vs Gaborone Leo 28/09/2025 Saa Ngapi?
- Ratiba ya Mechi za Leo 28/09/2025
- Singida Black Stars Yatinga Raundi Ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika
- Real Madrid Yapoteza 2-5 Dhidi ya Atletico Madrid, Kichapo cha Kwanza kwa Xabi Alonso LaLiga
- Haaland Sasa ni Miongoni mwa Wafungaji Bora 10 wa Muda Wote Man City
- Yanga Yatinga Raundi ya Pili CAF Champions League Baada ya Ushindi wa 2-0
- Matokeo ya Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025
- KMKM Yatinga Raundi ya Pili ya CAF Baada ya Kuichapa AS Port ya Djibouti
Leave a Reply