Matokeo ya Simba vs Petro De Luanda leo 23/11/2025
Simba SC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na rekodi thabiti katika michezo yao ya nyumbani ya CAF, licha ya kutopata ushindi kwenye mechi mbili za awali msimu huu dhidi ya Gaborone United (1–1) na Nsingizini Hotspurs (1–1).
Tangu ilipofungwa na Al Ahly bao 1–0 mnamo Machi 29, 2024, Simba haijapoteza mchezo wowote wa nyumbani kwenye michuano ya CAF, ikiwa imecheza mechi nane, kushinda tano na kutoka sare tatu.
Mpinzani wao, Petro de Luanda, anaingia dimbani akiwa na rekodi bora katika hatua za mtoano msimu huu. Timu hiyo imecheza mechi nne bila kupoteza, ikifunga jumla ya mabao 10 na kutoruhusu bao lolote, ikiwafunga Cercle de Joachim 6–0 na Stade d’Abidjan 4–0. Ukali wa safu yao ya ushambuliaji unaifanya Petro kuwa miongoni mwa timu zenye tishio kubwa.
Mchezo huu ni sehemu ya Kundi D linalohusisha timu za Simba, Petro de Luanda, Esperance de Tunis na Stade Malien.
Uchambuzi wa Rekodi za Timu
Simba SC
- Haijapoteza nyumbani kwenye CAF kwa zaidi ya mwaka mmoja.
- Mechi 8 mfululizo bila kupoteza nyumbani:
- Ushindi: 5
- Sare: 3
- Imepita hatua za mtoano kwa kuitoa Gaborone United (2–1) na Nsingizini Hotspurs (3–0).
- Malengo yao makuu msimu huu ni kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha Selemani Matola amesema kuwa mafanikio ya msimu huu yatategemea uwezo wa timu kutumia vizuri michezo ya nyumbani, akisisitiza: “Silaha yetu muhimu ni kutumia vyema mechi za nyumbani… hiyo ndiyo njia pekee itakayotubeba kufanikisha malengo yetu.”
Hata hivyo, Simba itawakosa mchezaji wake muhimu, kipa Moussa Camara, na beki Abdulrazack Hamza, ambao wana majeraha. Matola amekiri kuwa pengo hilo ni changamoto lakini maandalizi kwa ujumla yako vizuri.
Winga Joshua Mutale ameongeza kuwa wachezaji wote waliopo wako tayari kwa mchezo huu, akieleza:
“Tutajitoa kwa niaba ya mashabiki wetu ambao wamekuwa pamoja nasi katika kila hatua.”
Petro de Luanda
- Haijapoteza mchezo wowote katika hatua za mtoano msimu huu.
- Mechi nne, mabao 10, hakuna lililoruhusiwa.
- Imekuwa ikifanya vizuri hata ugenini.
- Rekodi ya misimu mitatu iliyopita kwenye CAF:
Makundi 2022–2023
Robo fainali 2023–2024
Hatua ya pili 2024–2025
Ukali wa washambuliaji wao unatabiri mchezo mgumu kwa Simba, hasa kutokana na uimara wao kwenye michuano ya Afrika.
Matokeo ya Simba vs Petro De Luanda leo 23/11/2025
Fuatilia matukio mbalimbali yatakayotokea wakati Simba SC ikikabiliana na Petro De Luanda katika mchezo wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Hapa tutakuletea taarifa za live kuhusu matokeo, magoli na zaidi.
| Simba Sc | VS | Petro De Luanda |
Kikosi cha Simba Kitakacho anza
Mapendekezo ya Mhariri








Leave a Reply