Matokeo ya Simba VS TRA United Leo 22/03/2026

Matokeo ya Simba VS TRA United Leo 22/03/2026

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo Jumapili Machi 22, 2026 wanatarajiwa kushuka dimbani kuikabili TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu NBC utakaopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es Salaam.

Mchezo huu unatajwa kuwa miongoni mwa mechi muhimu kabla ya mapumziko ya ligi kupisha kalenda ya FIFA, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona mwelekeo wa matokeo ya Simba vs TRA United leo 22/03/2026.

Matokeo ya Simba VS TRA United Leo 22/03/2026

Mchezo huu unawakutanisha Simba, ambao wanarejea nyumbani baada ya matokeo ya sare katika michezo yao ya hivi karibuni, dhidi ya TRA United, timu inayoonyesha ushindani mkubwa chini ya kocha Ettiene Ndayiragije.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, Simba imefanikiwa kushinda michezo miwili na kutoa sare tatu katika mechi tano zilizopita, huku TRA United nao wakishinda mbili, kupoteza mbili na kutoa sare moja dhidi ya Yanga. Takwimu hizi zinaonyesha uwezekano wa ushindani mkali katika dakika 90 za leo.

Kikosi cha Simba Kilichotangazwa

Simba imeingia kwenye mchezo huu ikiwa na kikosi chenye mchanganyiko wa uzoefu na nguvu mpya, kikiongozwa na nahodha Kapombe:

  • Kassali – golikipa
  • Kapombe (C) – beki na nahodha
  • Kibabage
  • Toure
  • De Reuck
  • Kagoma
  • Gueye
  • Clatous Chama
  • Seleman Mwalimu
  • Neo
  • Anicet Oura

Kurejea kwa mshambuliaji Seleman Mwalimu kunatajwa kuwa nyongeza muhimu kwa Simba, hasa katika kuboresha umaliziaji wa nafasi ambao umekuwa changamoto katika mechi zilizopita.

Matokeo ya Simba VS TRA United Leo 22/03/2026

Simba Sc 3-0 FT TRA United

Uchambuzi wa Kiufundi

Kocha wa Simba, Steve Barker, ameweka wazi dhamira ya kurejea kwenye ushindi, akisisitiza umuhimu wa kutumia vyema nafasi zinazotengenezwa. Kauli yake inaonyesha wazi kuwa Simba itaingia kwa mtazamo wa kushambulia huku ikihakikisha inakuwa makini katika safu ya ulinzi. Kwa upande wa TRA United, timu hiyo imeonyesha nidhamu ya hali ya juu, hususan katika mchezo wao dhidi ya Yanga. Uwezo wao wa kucheza kwa mpangilio na kutumia nafasi chache unaweza kuwa tishio kwa Simba.

Wachezaji wa Kuangaliwa

Simba itawategemea zaidi:

  • Clatous Chama – ubunifu wa mashambulizi
  • Anicet Oura – uwezo wa kubadili matokeo
  • Seleman Mwalimu – mshambuliaji kinara anayerudi kikosini

TRA United nao wanatarajiwa kuwategemea:

  • Ramadhani Chebwedo – mchezaji aliyeonyesha kiwango bora dhidi ya Yanga
    Joseph Akandwanaho – mshambuliaji hatari na kinara wa mabao

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  2. Matokeo ya Mtibwa Sugar vs Yanga Leo 21/03/2026
  3. Guinea Yadai Kombe Baada ya Morocco Kujiondoa Uwanjani 1976
  4. Hussein Katanga na Ally Mnyupe Wafungiwa Kwa Makosa ya Uamuzi wa Penalti
  5. Senegal Yapokonywa Ubingwa wa AFCON 2025 Baada ya CAF Kubadili Matokeo ya Fainali
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo