Matokeo ya Singida Black Star vs Yanga Leo 09/01/2026
Kikosi cha Young Africans SC leo kinashuka dimbani katika Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, kuwakabili Singida Black Stars katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Mapinduzi 2026, pambano lenye presha kubwa na lenye kuamua hatima ya timu zitakazotinga fainali ya michuano hiyo ya kihistoria.
Mchezo huu unapigwa leo Ijumaa, Januari 9, 2026, kuanzia saa 2:15 usiku, huku macho na masikio ya mashabiki wengi wa soka nchini yakielekezwa Zanzibar kushuhudia nani ataungana na mshindi wa nusu fainali ya kwanza kati ya Azam FC na Simba SC katika fainali itakayochezwa Januari 13, 2026, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Taarifa Kuhusu Mchezo wa Singoda Bis vs Yanga Leo
🏆 #mapinduzicupsemifinal
🆚 Singida BS
🗓️ 9 January 2026
🏟️ Amaan Complex
⏱️ Saa 2:15 Usiku
Matokeo ya Singida Black Star vs Yanga Leo 09/01/2026
| Singida Bs | 0-1 FT | Yanga Sc |
- 75’: Singida BS 0-1 Yanga SC (Maxi 53′)
View this post on Instagram
- 80’: Singida BS 0-1 Yanga SC (Maxi 53′)
Yanga ilikata tiketi ya nusu fainali baada ya ushindi mgumu wa bao 1-0 dhidi ya TRA United, ushindi ulioonyesha uimara wa kikosi hicho katika ulinzi na ushambuliaji. Kwa upande wao, Singida Black Stars walifuzu hatua hii baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya URA FC, matokeo yaliyowawezesha kukamilisha safari yao ya mafanikio katika hatua ya makundi.
Kwa kuzingatia mwenendo wa timu zote mbili, mchezo wa leo umebeba ushindani mkubwa kwani kila upande unaingia ukiwa na malengo makubwa ya kutinga fainali.
Kauli za Mabenchi ya Ufundi
Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji muhimu kutokana na majeraha. Ameeleza kuwa hali hiyo imewapa nafasi wachezaji wengine kuonyesha uwezo wao.
Kwa upande wa Singida Black Stars, Kocha Mkuu David Ouma amesisitiza nidhamu ya kiufundi kama silaha muhimu dhidi ya Yanga, timu inayojulikana kwa kasi na nguvu kubwa katika ushambuliaji. Ameeleza kuwa wakidhibiti mchezo vizuri, wanaamini wanaweza kufuzu kwenda fainali.
Mapendekezo ya Mhariri







Leave a Reply