Matokeo ya Yanga vs Al Ahly Leo 31/01/2026

Matokeo ya Yanga vs Al Ahly Leo 31/01/2026

Timu ya wananchi Yanga SC leo itashuka dimbani katika mtanange mkubwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wapinzani wao wa kihistoria Al Ahly, mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja. Macho ya mashabiki wa soka Tanzania yameelekezwa Zanzibar, ambako Yanga inapambana kurekebisha makosa waliyofanya katika mchezo wao wa awali na kulinda rekodi yake ya kutofungwa nyumbani dhidi ya mabingwa hao wa Afrika.

Mchezo huu ni miongoni mwa mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika zinazochezwa leo Jumamosi, lakini kwa Watanzania, pambano la Yanga dhidi ya Al Ahly ndilo lenye mvuto mkubwa zaidi kutokana na historia ndefu na ushindani mkali baina ya timu hizo mbili.

Katika msimamo wa sasa wa Kundi B, Al Ahly inaongoza kwa pointi saba, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi nne, huku AS FAR Rabat na JS Kabylie kila moja zikiwa na pointi mbili baada ya mechi tatu.

Matokeo ya Yanga vs Al Ahly leo yana uzito mkubwa katika mwelekeo wa kundi hili. Ushindi au hata sare kwa Yanga utaifanya ipande katika nafasi nzuri zaidi kuelekea kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa upande wa Al Ahly, pointi saba walizonazo zinawapa jeuri ya kusaka matokeo chanya ili kumaliza kinara wa kundi na kujihakikishia tiketi ya mapema ya robo fainali.

Historia ya Mikutano ya Yanga na Al Ahly

Yanga na Al Ahly zimekutana mara saba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye hatua mbalimbali. Rekodi za jumla zinaonyesha:

  • Al Ahly imeshinda mechi 4
  • Sare 2
  • Yanga imeshinda mechi 1

Matokeo ya mechi hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Yanga 1-0 Al Ahly (Machi 3, 2014)
  2. Al Ahly 1-0 Yanga (Machi 9, 2013 – Al Ahly ikashinda penalti 4-3)
  3. Yanga 1-1 Al Ahly (Aprili 9, 2016)
  4. Al Ahly 2-1 Yanga (Aprili 20, 2016)
  5. Yanga 1-1 Al Ahly (Desemba 2, 2023)
  6. Al Ahly 1-0 Yanga (Machi 1, 2024)
  7. Al Ahly 2-0 Yanga (Januari 23, 2026)

Cha kufurahisha ni kwamba, Yanga haijawahi kufungwa nyumbani dhidi ya Al Ahly. Kwenye ardhi ya Tanzania, Yanga ina rekodi ya ushindi mmoja na sare mbili.

Mara ya mwisho Yanga kuikaribisha Al Ahly nyumbani ilikuwa Desemba 2, 2023, ambapo mechi ilimalizika kwa sare ya 1-1.

Matokeo ya Yanga vs Al Ahly Leo 31/01/2026

Yanga Sc VS Al Ahly

Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Al Ahly

Kikosi cha Kuanza

  1. Diarra
  2. Job
  3. Boka
  4. Mwamnyeto
  5. Bacca
  6. Damaro
  7. Maxi
  8. Abuya
  9. Depu
  10. Zouzoua
  11. Okello

Wachezaji wa Akiba; Mshery, Mwenda, Hussein, Assinki, Mudathir, Shekhani, Emma, Lassine & Dube

Changamoto na Mbinu za Timu

Kipigo cha 2-0 ambacho Yanga ilipokea ugenini Januari 23, 2026 kimeongeza presha na hamasa ndani ya kikosi hicho kuelekea mchezo wa leo. Upinzani walioutoa ugenini licha ya kupoteza, umeonyesha kwamba Yanga ina uwezo wa kupambana, hasa kama itarekebisha maeneo mawili muhimu: ulinzi na umaliziaji wa nafasi.

Kwa upande wake, Al Ahly inapocheza ugenini katika hatua za makundi, huwa haitumii mbinu za kushambulia sana. Mara nyingi hulenga zaidi kuzuia na kusubiri makosa ya wapinzani, jambo ambalo limeifanya ipate matokeo chanya ilipokuja Tanzania.

Mchango wa Laurindo Depu

Mmoja wa wachezaji wanaozungumziwa zaidi ndani ya kikosi cha Yanga ni Laurindo Depu, ambaye ameonyesha kiwango kizuri tangu ajiunge na timu hiyo.

Katika mechi tatu alizocheza:

Amefunga mabao 3

Amefanya asisti 1

Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, alinukuliwa akisema kuwa:

“Kile anachokifanya Depu kwa sasa ni kama asilimia 35 ya uwezo wake halisi.”

Kauli hiyo imeongeza matumaini kwa mashabiki wa Yanga, kwamba endapo Depu ataendelea kuzoea mfumo wa timu, anaweza kuwa silaha muhimu dhidi ya Al Ahly.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. CV Ya Anicet Oura Mshambuliaji Mpya wa Simba 2025/2026
  2. Msimamo wa Kundi la Singida Bs Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
  3. Msimamo wa Kundi la Azam Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
  4. Msimamo Kundi la Simba Klabu Bingwa 2025/2026
  5. Msimamo Kundi la Yanga Klabu Bingwa 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo