Matokeo ya Yanga VS Mashujaa Leo 19/01/2026
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo Jumatatu wanarejea tena katika ushindani wa ligi hiyo kwa kushuka dimbani kumenyana na Mashujaa FC katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Mechi hii ya Ligi Kuu Bara inapigwa katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni, huku macho ya mashabiki yakielekezwa kuona matokeo ya Yanga VS Mashujaa leo 19/01/2026. Mchezo huo utarushwa moja kwa moja kupitia Azam Sports 1 HD, hatua inayowapa fursa mashabiki walioko ndani na nje ya uwanja kufuatilia pambano hilo muhimu.
Yanga SC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na dhamira ya kuendeleza mwenendo mzuri ilionao tangu kuanza kwa msimu. Timu hiyo inahitaji ushindi ili kuendelea kubaki juu ya msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kufikisha pointi 19, baada ya kucheza mechi sita, huku JKT Tanzania ikiwa na pointi 17 baada ya michezo 10.
Chini ya kocha Pedro Goncalves, Yanga imeonyesha uimara mkubwa. Tangu ajiunge na klabu hiyo Novemba 5, 2025, Pedro ameiongoza Yanga katika mechi tisa za mashindano mbalimbali na hajapoteza hata mchezo mmoja. Katika kipindi hicho, Yanga imeshinda mechi nane na kupata sare moja.
Katika mechi hizo, Yanga imeshinda michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara, michezo minne ya Kombe la Mapinduzi 2026, mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi na kupata sare moja katika mashindano hayo ya Afrika.
Nyota Wapya Waanza Kuonyesha Makali
Machoni pa mashabiki wengi, macho yatakuwa kwa Emmanuel Mwanengo na Mohamed Damaro, ambao tayari wameanza kujitambulisha ndani ya kikosi cha Yanga. Wachezaji hao walionyesha kiwango bora katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2026, ambapo Yanga ilitwaa taji hilo baada ya kuifunga Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4.
Wakati Mwanengo na Damaro wakiendelea kung’ara, Okello na Depu bado walionekana kuendelea na mazoezi ya pamoja na wenzao. Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa kuwa leo Jumatatu wakaanza rasmi safari yao ya Ligi Kuu Bara endapo mambo yatakwenda kama ilivyopangwa.
Fuatilia Hapa Matokeo ya Yanga VS Mashujaa Leo 19/01/2026
| Yanga | VS | Mashujaa |
🏆 #nbcpremierleague
🆚 Mashujaa FC
🗓️ 19 January 2026
🏟️ KMC Complex, Mwenge
⏱️ Saa 10:00 Jioni
Rekodi Zamlazimu Mashujaa Kuwa Makini
Kwa upande wa Mashujaa FC kutoka Kigoma, mchezo huu ni fursa ya kusaka matokeo chanya ili kufikisha pointi 16 na kusogea juu zaidi kwenye msimamo wa ligi. Hata hivyo, rekodi za nyuma haziwapi matumaini makubwa.
Huu ukiwa msimu wa tatu kwa Mashujaa kushiriki Ligi Kuu Bara, timu hiyo haijawahi kupata hata sare mbele ya Yanga. Katika mechi zote walizokutana, Mashujaa imekuwa ikipoteza, iwe nyumbani au ugenini.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika Uwanja wa KMC Complex ilikuwa Desemba 19, 2024, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2. Baadaye, Februari 23, 2025, Yanga ilipata ushindi mnono wa mabao 5-0 ilipokuwa ugenini nyumbani kwa Mashujaa.
Katika msimu wa 2024, timu hizo zilianza kukutana Februari 8, ambapo Yanga ilishinda 2-1 nyumbani, kabla ya kurejea na ushindi wa bao 1-0 ugenini Mei 5, 2024.
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply