Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025

Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 | Matokeo ya Yanga leo Dhidi ya Singida Black Stars Fainali

Timu ya Wananchi, Yanga SC, inatarajiwa kushuka tena dimbani leo Jumapili, tarehe 29 Juni 2025, kuwania taji la Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup, ikiwa ni baada ya kukamilisha rasmi safari ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC mnamo tarehe 25 Juni kwa kuichapa Simba SC mabao 2-0. Fainali ya leo dhidi ya Singida Black Stars imepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 2:15 usiku (20:15), ikiwa ndiyo mchezo wa mwisho wa msimu wa 2024/2025 kwa klabu zote mbili.

Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 – Nini Kinasubiriwa?

Mchezo huu wa fainali unatarajiwa kuwa wa ushindani mkali kati ya mabingwa watetezi Yanga na Singida BS wanaosaka taji lao la kwanza la kitaifa. Wakati mashabiki wakisubiri matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars leo 29/06/2025, macho yote yataelekezwa Zanzibar, ambako historia mpya inaweza kuandikwa baada ya dakika 90 au zaidi ikiwa kutahitajika muda wa nyongeza au mikwaju ya penalti.

Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025

Fuatilia Hapa Matokeo ya Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Pindi Mchezo Utakapo Anza

Yanga Sc VS Singida Black Stars

 

Kuelekea Fainali – Vikosi na Mbinu za Makocha

Yanga SC, chini ya kocha Miloud Hamdi, wanapanga kuendeleza rekodi yao nzuri kwenye mashindano haya kwa kutegemea uti wa mgongo wa timu unaojumuisha viungo waliobobea kama Khalid Aucho, Duke Abuya na Mudathir Yahya. Washambuliaji wanaotarajiwa kuibeba timu ni Pacome Zouzoua, Prince Dube, Maxi Nzengeli na Clement Mzize.

Kwa upande wa Singida Black Stars, kocha David Ouma amekiandaa kikosi chake kwa umakini mkubwa, akiwategemea wachezaji wake wa kigeni walioweka rekodi nzuri ya kufunga mabao katika hatua za awali. Jonathan Sowah, mshambuliaji kinara wa timu hiyo, ataongoza safu ya mbele pamoja na wachezaji kama Emmanuel Keyekeh, Marouf Tchakei na Victorien Adebayor.

Safari ya Kufika Fainali – Takwimu Muhimu

Yanga imecheza mechi tano kuelekea fainali na kufunga mabao 20, huku wakiruhusu mabao mawili pekee. Safu yao ya ushambuliaji imekuwa tishio, ikiongozwa na wageni walioweka mabao 15, na wazawa wakifunga matano.

Singida Black Stars wamefunga mabao 12 katika mechi tano, ambapo mabao 11 yamefungwa na wachezaji wa kigeni. Kwa rekodi hiyo, fainali hii inaweza kuamua nani ana safu kali zaidi ya ushambuliaji na ulinzi imara.

Historia, Rekodi na Kisasi

Yanga SC wanaingia katika fainali hii wakiwa hawajapoteza mechi yoyote ya Kombe la FA tangu Julai 2021, wakiwa na rekodi ya kucheza fainali tano mfululizo, na tayari wameshinda mara nne tangu msimu wa 2015-2016.

Kwa Singida Black Stars, hii ni fursa ya kuweka historia ya kwanza kwa klabu hiyo. Timu hii bado haijawahi kushinda taji lolote kubwa, na kushinda leo kutakuwa hatua kubwa ya mafanikio kwao.

Msimu huu, timu hizi zimekutana mara mbili kwenye Ligi Kuu, ambapo Yanga ilishinda mechi zote bila kuruhusu bao: 1-0 na 2-0. Hivyo Singida Black Stars wanalenga si tu taji, bali pia kuvunja rekodi ya kutofunga dhidi ya Yanga msimu huu.

Matarajio Ya Mchezo – Saa 2:15 Usiku Zanzibar

Fainali hii inatarajiwa kuchezwa kwa kasi na nidhamu ya hali ya juu, ikizingatiwa uzoefu wa makocha wote wawili. Miloud Hamdi, ambaye aliwahi kuifundisha Singida mwishoni mwa mwaka 2024 kabla ya kujiunga na Yanga, atakuwa na nia ya kutwaa taji la pili msimu huu akiwa na klabu hiyo. Kwa upande mwingine, David Ouma wa Singida anataka kufanikisha malengo yake ya kuifikisha timu hiyo kileleni kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa mwenendo wa mechi zao zilizopita, mabao mengi yanatarajiwa kufungwa kipindi cha pili. Yanga imekuwa na uwiano sawa wa mabao kipindi cha kwanza na pili, ilhali Singida imekuwa tishio zaidi kipindi cha pili.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Fainali ya CRDB Saa Ngapi?
  2. Kikosi cha Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Fainali ya CRDB
  3. Ratiba ya Fainali ya CRDB Federation Cup 2025
  4. Chelsea Yajipanga Kuzima Moto wa Di Maria Katika Mechi ya Usiku Dhidi ya Benfica
  5. Simba Yavizia Saini ya Issa Fofana Nchini Ivory Coast Kama Mrithi wa Camara
  6. Ratiba ya CHAN 2024/2025 | CAF African Nations Championship
  7. Ratiba ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025 Hatua ya 16 Bora
  8. Form Five Selection 2025: Majina Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 Yatangazwa!
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo