Matokeo ya Yanga vs Tanzania Prisons Leo 04/04/2026
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, wameshuka dimbani leo Jumamosi Aprili 4, 2026 wakiwa na shinikizo kubwa la kusaka ushindi mbele ya Tanzania Prisons katika mchezo unaovuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini.
Huu ni mchezo unaokuja kipindi ambacho Yanga wanahitaji kurejesha makali yao baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha, huku Tanzania Prisons nao wakiingia uwanjani wakitafuta pointi muhimu za kujinasua kutoka sehemu za chini za msimamo. Kwa uzito wa mechi hii, macho mengi yameelekezwa si tu kwenye matokeo ya uwanjani, bali pia kwenye kikosi rasmi kilichoanzishwa na benchi la ufundi la Wananchi.
Kikosi rasmi cha Yanga SC leo
Kocha wa Yanga ameanza mchezo huu kwa kikosi chenye mchanganyiko wa uzoefu na nguvu ya ushambuliaji, huku baadhi ya majina muhimu yakiongoza safu mbalimbali.
Kikosi cha kwanza (Starting XI):
- 16 Msher y
- 33 Mwenda
- 15 Hussein
- 4 Bacca
- 38 Assink
- 38 Abuya (C)
- 7 Maxi
- 27 Mudathir
- 10 Pacome
- 20 Okello
- 13 Buba
Wachezaji wa akiba: Masalanga, Kibwana, Yao, Abubakar, Damaro, Kouma, SureBoy, Andabwile, Abdulnassir, Sheikhan
Taarifa hizi zinaendana na mabadiliko ya kikosi kuelekea mchezo huu ambapo baadhi ya nyota wamepewa nafasi huku wengine wakianzia benchi.
Fuatilia Hapa Matokeo ya Yanga vs Tanzania Prisons Leo 04/04/2026
| Yanga Sc | Vs | Tanzania Prisons |
🏆 #NBCPremierLeague
Yanga Sc🆚 Tanzania Prisons
🗓️ 04 April 2026
🏟️ KMC Complex
⏱️ 12:30 Jioni
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply