Mechi ya Pili ya Dabi ya Kariakoo Simba vs Yanga Kuchezwa Desemba 13 2025

Mechi ya Pili ya Dabi ya Kariakoo Simba vs Yanga Kuchezwa Desemba 13 2025

Watani wa jadi Simba na Yanga sasa ni rasmi watakutana mara mbili ndani ya miezi mitatu ya mwanzo wa msimu wa 2025/2026. Kwa mara ya kwanza, mashabiki wa soka nchini watashuhudia pambano la fainali ya Ngao ya Jamii litakalopigwa tarehe 16 Septemba 2025. Kisha, mechi ya pili ya Dabi ya Kariakoo Simba vs Yanga kuchezwa Desemba 13, 2025 katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Hii inakuwa mara ya kwanza kwa mashabiki kupata ladha ya mikikimikiki ya watani hawa kabla ya msimu kuingia katika kipindi cha mapumziko ya Krismasi.

Mechi ya Pili ya Dabi ya Kariakoo Simba vs Yanga Kuchezwa Desemba 13 2025

Yanga Kuwa Mwenyeji wa Dabi ya Pili

Kwa mujibu wa ratiba rasmi iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) Agosti 29, 2025, mechi ya Desemba 13 itakuwa ya duru ya kwanza kati ya watani hao, ambapo Yanga itaingia uwanjani kama mwenyeji dhidi ya Simba. Hii inatarajiwa kuwa moja ya mechi zenye ushindani mkubwa kutokana na historia ya mechi za awali ambazo mara zote zimekuwa zikivuta maelfu ya mashabiki ndani na nje ya uwanja.

Ratiba ya Ligi Kuu NBC 2025/2026

Bodi ya Ligi kupitia Kaimu Mtendaji Mkuu wake, Ibrahim Mwayela, imethibitisha kuwa msimu mpya wa Ligi Kuu utaanza rasmi Septemba 17, 2025. Katika siku ya ufunguzi, michezo miwili itapigwa:

KMC dhidi ya Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.

Coastal Union dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kwa mujibu wa TPLB, ratiba hiyo imetengenezwa kwa uangalifu mkubwa ili kuzingatia mashindano ya ndani na ya kimataifa, ikiwemo michuano ya CHAN 2025 ambayo Tanzania ni mwenyeji.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba Yamtambulisha Selemani Mwalimu Kutoka Wydad AC kwa Mkopo wa Mwaka
  2. Simba Kuivaa Gor Mahia ya Kenya Kwenye Kilele cha Simba Day
  3. Mshambuliaji Clement Mzize Asaini Kuendelea na Yanga Hadi 2027
  4. Opah Clement Atambulishwa Rasmi SD Eibar ya Hispania
  5. Yanga SC Kucheza Dhidi ya Bandari FC Siku ya Wiki ya Mwananchi
  6. Morocco Yatinga Fainali ya CHAN Baada ya Kuifunga Senegal kwa Penalti
  7. Madagascar Kukipiga Dhidi ya Morocco Fainali ya CHAN 2025
  8. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo