Mohamed Hussein Shabalala Ajiunga na Yanga SC Baada ya Miaka 11 Simba

Mohamed Hussein Shabalala Ajiunga na Yanga SC Baada ya Miaka 11 Simba

Nyota wa zamani wa Klabu ya Simba SC, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’, sasa ni rasmi kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga SC kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026. Beki huyo wa kushoto ametambulishwa rasmi na Wananchi baada ya kumaliza huduma yake ya muda mrefu ndani ya wekundu wa Msimbazi, Simba SC, ambapo alihudumu kwa miaka 11 mfululizo.

Ujio wa Mohamed Hussein ndani ya Yanga SC umeibua mjadala mpana katika medani ya soka la Tanzania, hasa ikizingatiwa kuwa amejiunga na watani wa jadi wa klabu yake ya zamani. Hatua hii inamweka kwenye orodha ya wachezaji wachache waliowahi kucheza katika klabu mbili kubwa za soka nchini, Simba na Yanga, kwa vipindi tofauti vya maisha yao ya soka.

Mohamed Hussein Shabalala Ajiunga na Yanga SC Baada ya Miaka 11 Simba

Beki Mwenye Historia Kwenye Soka la Tanzania

Mohamed Hussein, maarufu kwa jina la Zimbwe Jr, anafahamika kwa uwezo wake wa kulinda eneo la kushoto la uwanja, nidhamu ya hali ya juu, pamoja na uzoefu mkubwa katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Akiwa Simba SC, alikua chaguo la kwanza katika nafasi ya beki wa kushoto kwa zaidi ya muongo mmoja, akitoa mchango mkubwa kwa mafanikio ya klabu hiyo kwenye Ligi Kuu, Kombe la FA na mashindano ya CAF.

Kwa kujiunga na Yanga SC, Zimbwe Jr anatarajiwa kuleta ushindani mpya katika safu ya ulinzi ya Wananchi, huku benchi la ufundi likiwa na matarajio makubwa kutokana na uzoefu na umahiri wa mchezaji huyo ndani ya uwanja.

Anaungana na Majina Makubwa Waliozitumikia Simba na Yanga

Mohamed Hussein anaingia kwenye historia ya wachezaji waliowahi kuichezea Simba na Yanga, klabu zinazotambuliwa kama miamba ya soka la Tanzania. Katika orodha hii wamo mastaa waliowahi kufanya hivyo kwa mafanikio, akiwemo:

  1. Clatous Chama
  2. Israel Mwenda
  3. Bernard Morrison
  4. Mrisho Ngassa
  5. Haruna Niyonzima
  6. Saidi Ntibazonkiza
  7. Juma Kaseja
  8. Jonas Mkude
  9. Emmanuel Okwi
  10. Kelvin Yondani

Hatua ya Shabalala kuhamia Yanga SC inaonekana kuwa sehemu ya mikakati ya klabu hiyo kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao, huku mashabiki wakisubiri kuona athari ya usajili huu kwenye uwanja wa mapambano.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya CHAN 2025 Mechi za Makundi
  2. Msimamo Kundi la Tanzania CHAN 2024
  3. Orodha ya Wachezaji Wazawa Yanga Sc 2025/2026
  4. CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026
  5. Cv ya Mohammed Bajaber Kiungo Mshambuliaji Mpya Simba Sc 2025/2026
  6. Picha za Wachezaji Wapya wa Simba 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo