Mshahara Wa Stephane Aziz Ki Yanga 2024/2025
Baada ya kuwako na uvumi kua Stephane Aziz Ki hajasaini mkataba mpya na Yanga na kuwa wapo wengi wanaosubiri kuona kama mchezaji huyu ataondoka Yanga huku kukiwa na vilabu vikubwa nje vikiripotiwa kutaka saini ya nyota huyo, hatimaye leo Julai 10, 2024, Yanga imetangaza rasmi kusaini mkataba mpya na Aziz Ki, ambaye ataendelea kuichezea klabu ya Yanga msimu wa 2024/2025.
Stephane Aziz Ki ni mchezaji muhimu kwa Yanga SC, akiwa na nafasi kubwa katika mafanikio ya klabu. Kumbakisha Stephane Aziz Ki ni habari kubwa na muhimu kwa Yanga, licha ya kuongeza mikataba ya wachezaji nane na pia kusaini nyota kadhaa wapya katika dirisha kubwa la usajili linaloendelea.
Katika msimu uliopita, Aziz Ki alionyesha kiwango bora sana, akifunga mabao 21 kwenye Ligi Kuu na kupiga pasi za mwisho nane, na kuiwezesha Yanga kutwaa ubingwa huku yeye akiibuka mfungaji bora. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, alihusika na mabao manne katika mechi 12, akifunga mabao mawili na kupiga pasi mbili za mwisho, na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya robo fainali.
Ofa zilizopo mezani kutoka kwa timu mbalimbali, historia ya kuamua matokeo ya mechi kubwa, pamoja na ushawishi mkubwa alionao kwa vigogo wa timu hiyo, ni mambo ambayo yameishawishi Yanga kuhakikisha wanambakisha mchezaji huyo raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 28. Timu nyingi ndani na nje ya bara la Afrika, zikiwemo Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns, na Orlando Pirates, zimeonesha nia ya kumsajili mchezaji huyu. Kwa mashabiki wa Yanga, kumbakisha Stephane Aziz Ki ni ishara ya uhakika kwamba klabu itaendelea kuwa na nguvu katika ligi na mashindano mbalimbali.
Mshahara Wa Stephane Aziz Ki Yanga 2024/2025
Stephane Aziz Ki ataendelea kubaki Yanga baada ya kukubaliana na klabu kuongeza mkataba ambao unasemekana utamfanya kua ni moja kati ya wachezaji wanaolipwa pesa ndefu Tanzania. Mkataba mpya wa Aziz Ki Yanga unasemekana kua Mastar Key atapokea mshahara unaokadiriwa kufikia dola 13,000 (sawa na shilingi milioni 35) kwa mwezi kwa msimu wa 2024/2025.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti