Msimamo wa Makundi ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025
Michuano ya Kombe la Dunia ya Vilabu hatimaye inaanza kutimua vumbi Jumamosi mapema kabisa huko Marekani, ikiwaleta pamoja vigogo 32 kutoka mabara sita duniani katika mfumo mpya kabisa wa mashindano unaotarajiwa kutoa burudani ya kipekee kwa mashabiki wa soka kote duniani. Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake, michuano hii ya FIFA Club World Cup itafanyika kwa mtindo wa Kombe la Dunia, ikifanyika kila baada ya miaka minne na kuwajumuisha washiriki 32 badala ya saba kama ilivyokuwa awali. Marekani ikiwa mwenyeji wa toleo hili la kihistoria, itakuwa jukwaa la timu bora kutoka kila bara kuonesha ubabe wao.
Mfumo Mpya wa Mashindano
Mashindano ya mwaka 2025 yanakuja na sura mpya – timu 32, makundi 8, kila kundi likiwa na timu 4. Kila timu ilijipatia nafasi kwa kushinda au kufanya vizuri katika mashindano ya vilabu ya mabara yao kati ya msimu wa 2020-21 hadi 2023-24.
Ugawaji wa Nafasi kwa Mabara:
- Ulaya (UEFA): Timu 12 (ndiyo yenye wawakilishi wengi zaidi)
- Amerika Kusini (CONMEBOL): Timu 6
- Asia (AFC): Timu 4
- Afrika (CAF): Timu 4
- Amerika ya Kaskazini & Kati (CONCACAF): Timu 4 + 1 (nafasi ya mwenyeji – Marekani)
- Oceania (OFC): Timu 1
Miongoni mwa vilabu vya Ulaya vilivyofanikiwa kufuzu ni Chelsea, Manchester City, Real Madrid, PSG, Bayern Munich, Juventus, Benfica, na Atlético Madrid. Red Bull Salzburg, maarufu kama FC Salzburg, pia wamejipatia nafasi kupitia mfumo wa alama kwa nchi zisizojaza nafasi mbili.
Msimamo wa Makundi ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025
Kwa sasa, kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, msimamo wa makundi ni wa awali na hakuna mechi iliyochezwa. Hapa chini ni muundo wa makundi yote nane:
Kundi A
- Al Ahly
- Inter Miami
- Palmeiras
- Porto
Kundi B
- Atlético Madrid
- Botafogo
- Paris Saint-Germain (PSG)
- Seattle Sounders
Kundi C
- Auckland City
- Bayern Munich
- Benfica
- Boca Juniors
Kundi D
- Chelsea
- ES Tunis
- Flamengo
- Club León
Kundi E
- Inter Milan
- Monterrey
- River Plate
- Urawa Red Diamonds
Kundi F
- Borussia Dortmund
- Fluminense
- Mamelodi Sundowns
- Ulsan Hyundai
Kundi G
- Al Ain
- Juventus
- Manchester City
- Wydad Athletic Club
Kundi H
- Al-Hilal
- Pachuca
- Real Madrid
- RB Salzburg (FC Salzburg)
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba Kususia Dabi Nyingine Kama Yanga Hawatoshiriki Mchezo wa June 15
- Timu Zilizofuzu Nusu Fainali COSAFA Cup 2025
- Taifa Stars Yaaga COSAFA Cup Licha ya Kuifunga Eswatini 2-1
- Tijjani Reijnders Asaini Manchester City Miaka Mitano Akitokea AC Milan
- Serikali Yajieka Pembeni na Sakata la dabi, yawaachia TFF
- Chelsea Yathibitisha Kumsajili Beki Mamadou Sarr Kutoka Strasbourg
- Yanga Kususia Fainali CRDB FA Cup Kisa Madeni ya Msimu Uliopita
- Yanga Yaibua Mambo Mapya Wakizungumzia Sakata la Dabi
Leave a Reply