Nafasi Mpya 10026 za Kazi Walimu MDAs & LGAs 2025
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea (MDAs) na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) ametangaza nafasi mpya 10,026 za kazi za Ualimu katika fani mbalimbali kwa mwaka 2025. Tangazo hili linatoa fursa kwa watanzania wenye sifa stahiki kuomba nafasi hizo ili kujaza upungufu wa walimu katika taasisi za elimu nchini.
Tangazo hili linahusisha nafasi kwa walimu wa masomo ya Sayansi, Sanaa, na Ufundi, zikiwa zimegawanywa katika madaraja tofauti kulingana na taaluma na kiwango cha elimu. Walimu wanaotaka kujiunga na ajira hizi wanahimizwa kuzingatia masharti na utaratibu wa maombi kama ulivyoelekezwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Orodha ya Nafasi Mpya za Kazi kwa Walimu 2025
Zifuatazo ni baadhi ya nafasi zilizotangazwa chini ya tangazo la Nafasi Mpya 10026 za Kazi Walimu MDAs & LGAs 2025:
- Mwalimu Daraja la III C (Kemia) – Nafasi 682
- Mwalimu Daraja la III B (Kemia) – Nafasi 257
- Mwalimu Daraja la III C (Kilimo) – Nafasi 171
- Mwalimu Daraja la III B (Kilimo) – Nafasi 64
- Mwalimu Daraja la III B (Fizikia) – Nafasi 433
- Mwalimu Daraja la III C (Fizikia) – Nafasi 1,148
- Mwalimu Daraja la III C (Historia) – Nafasi 124
- Mwalimu Daraja la III C (TEHAMA) – Nafasi 168
- Mwalimu Daraja la III B (TEHAMA) – Nafasi 64
- Mwalimu Daraja la III B (Hisabati) – Nafasi 709
- Mwalimu Daraja la III C (Hisabati) – Nafasi 1,883
- Mwalimu Daraja la III C (Jiografia) – Nafasi 96
- Mwalimu Daraja la III C (Kiswahili) – Nafasi 144
- Mwalimu Daraja la III C (Baiolojia) – Nafasi 1,218
- Mwalimu Daraja la III B (Baiolojia) – Nafasi 459
- Mwalimu Daraja la III C (Food and Human Nutrition) – Nafasi 37
- Mwalimu Daraja la III B (Food and Human Nutrition) – Nafasi 14
- Mwalimu Daraja la III B – Shule ya Msingi – Nafasi 1,000
- Mwalimu Daraja la III C (Kiingereza) – Nafasi 235
- Fundi Sanifu Daraja la II (Umeme) – Nafasi 36
- Msaidizi Afya ya Mazingira II – Nafasi 219
- Msaidizi wa Misitu Daraja la II – Nafasi 13
- Mkadiri Ujenzi Daraja la II (Quantity Surveyor) – Nafasi 97
- Fundi Sanifu Mkadiriaji Majenzi Daraja la II – Nafasi 1
- Mwalimu Daraja la III C (Animal Health Production) – Nafasi 6
- Mwalimu Daraja la III C (Autobody Repair) – Nafasi 8
- Mwalimu Daraja la III C (Useremala) – Nafasi 10
- Mwalimu Daraja la III C (Computer Programming) – Nafasi 5
- Mwalimu Daraja la III C (Designing, Sewing and Cloth Technology) – Nafasi 1
- Mwalimu Daraja la III C (Graphics Designing) – Nafasi 2
- Mwalimu Daraja la III C (Horticulture Production) – Nafasi 2
- Mwalimu Daraja la III C (Hair Dressing) – Nafasi 1
- Mwalimu Daraja la III C (Fitter Mechanics) – Nafasi 7
- Mwalimu Daraja la III C (Masonry and Bricklaying) – Nafasi 1
- Mwalimu Daraja la III C (Meat Processing) – Nafasi 1
- Mwalimu Daraja la III C (Food and Beverage, Sales and Services) – Nafasi 1
- Mwalimu Daraja la III C (Netball Performance) – Nafasi 13
- Mwalimu Daraja la III C (Handloom Weaving) – Nafasi 1
- Mwalimu Daraja la III C (Plumbing) – Nafasi 16
- Mwalimu Daraja la III C (Welding and Metal Fabrication) – Nafasi 10
- Mwalimu Daraja la III C (Motor Vehicle Mechanics) – Nafasi 11
- Mwalimu Daraja la III C (Track Event) – Nafasi 6
- Mwalimu Daraja la III C (Historia ya Tanzania na Maadili) – Nafasi 270
- Mwalimu Daraja la III C (Biashara) – Nafasi 381
- Mwalimu Daraja la III C (Ngoma) – Nafasi 1
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeweka masharti maalum kwa waombaji wote wa nafasi hizi za kazi. Waombaji wanapaswa kusoma kwa makini masharti yafuatayo kabla ya kuwasilisha maombi yao:
- Waombaji wote lazima wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45, isipokuwa wale walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu katika mfumo wa maombi.
- Waombaji waambatishe CV iliyo kamili yenye maelezo binafsi, anuani, namba za simu, na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
- Kila mwombaji lazima aambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waajiriwa wa Umma hawaruhusiwi kuomba, isipokuwa kwa kuzingatia maelekezo ya waraka rasmi wa Serikali.
- Maombi yaambatane na vyeti vya elimu vilivyothibitishwa, ikiwemo vyeti vya kidato cha IV, kidato cha VI, na vyeti vya kitaaluma vinavyohusiana na kazi.
- Hati za matokeo, “provisional results,” au “testimonials” hazitakubaliwa kama nyaraka rasmi.
- Waombaji waliosoma nje ya nchi lazima wahakikishe vyeti vyao vimeidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NECTA, au NACTE.
- Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Kuwasilisha taarifa za uongo au kughushi kutasababisha hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 01 Novemba 2025.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wote wanapaswa kutuma maombi yao kupitia mfumo rasmi wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) unaopatikana kupitia tovuti rasmi: 👉 https://portal.ajira.go.tz
Aidha, barua ya maombi lazima ielekezwe kwa:
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S.L.P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatazingatiwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025
- Majina ya Waliochaguliwa Kusimamia Uchaguzi 2025
- Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo ya Kusimamia Uchaguzi INEC 2025 Mkoa wa Singida
- Ajira Mpya za Walimu MDAs & LGAs 2025: Nafasi 3018 za Mwalimu Daraja la IIIA Zatangazwa
- Majina ya Waliochaguliwa Kusimamia Uchaguzi 2025 Kigamboni
- Mfano Wa Barua Ya Kuomba Kazi Mwalimu Daraja La IIIA
Leave a Reply