Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025

Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali (MDAs) pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs), ametangaza rasmi nafasi mpya za kazi 17,710 kwa Watanzania wenye sifa, ujuzi na uwezo wa kujaza nafasi hizo.

Tangazo hili, lililotolewa tarehe 16 Oktoba 2025, linahusisha kada mbalimbali katika sekta za afya, kilimo, utawala, elimu, uhasibu, mifugo, uhandisi na nyingine nyingi kote nchini. Sekretarieti ya Ajira inasisitiza kuwa ajira hizi ni fursa muhimu kwa Watanzania wenye sifa stahiki kuchangia katika maendeleo ya taifa kupitia ajira za umma.

Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025
Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025

Orodha ya Nafasi Mpya za Kazi (MDAs & LGAs October 2025)

Ifuatayo ni orodha kamili ya nafasi zote 17,710 zilizotangazwa katika tangazo la Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025:

  • Mhasibu Daraja la II (Accountant Grade II) – Nafasi 131
  • Afisa Ukuzaji Viumbe Kwenye Maji Msaidizi Daraja la II (Assistant Aquaculture Officer Grade II) – Nafasi 1
  • Msaidizi wa Hesabu Daraja la II (Accounts Assistant Grade II) – Nafasi 126
  • Afisa Tawala Daraja la II (Administrative Officer Grade II) – Nafasi 32
  • Afisa Hesabu Daraja la II (Accounts Officer II) – Nafasi 224
  • Mhandisi Kilimo Daraja la II (Agro Engineer Grade II) – Nafasi 24
  • Afisa Uvuvi Msaidizi Daraja la II (Assistant Fisheries Officer II) – Nafasi 35
  • Afisa Kilimo Msaidizi Daraja la II (Agricultural Field Officer II) – Nafasi 292
  • Afisa Kilimo Msaidizi Daraja la III (Agricultural Field Officer III) – Nafasi 76
  • Mkufunzi Daraja la II – Kilimo (Agricultural Officer Grade II) – Nafasi 73
  • Fundi Sanifu Daraja la II – Kilimo (Agricultural Technician Grade II) – Nafasi 15
  • Afisa Ukuzaji Viumbe Kwenye Maji Daraja la II (Aquaculture Officer Grade II) – Nafasi 3
  • Msanifu Majengo Daraja la II (Architect Grade II) – Nafasi 62
  • Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daraja la II (Assistant Game & Sports Development Officer Grade II) – Nafasi 7
  • Afisa Ufugaji Nyuki Msaidizi Daraja la II (Assistant Beekeeping Officer II) – Nafasi 5
  • Afisa Mlezi wa Watoto Msaidizi Daraja la II (Assistant Child Care Officer Grade II) – Nafasi 5
  • Afisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi Daraja la II (Assistant Community Development Officer II) – Nafasi 179
  • Afisa Utamaduni Msaidizi (Assistant Cultural Officer Grade II) – Nafasi 1
  • Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II (Assistant Environmental Health Officer Grade II) – Nafasi 161
  • Afisa TEHAMA Msaidizi Daraja la II (Assistant ICT Officer Grade II) – Nafasi 35
  • Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II (Assistant Nursing Officer Grade II) – Nafasi 3,945
  • Afisa Ununuzi Msaidizi Daraja la II (Assistant Procurement Officer Grade II) – Nafasi 16
  • Afisa Ustawi wa Jamii Msaidizi Daraja la II (Assistant Social Welfare Officer Grade II) – Nafasi 76
  • Afisa Ugavi Msaidizi Daraja la II (Assistant Supplies Officer Grade II) – Nafasi 18
  • Msaidizi wa Ufugaji Nyuki Daraja la II (Beekeeping Assistant Grade II) – Nafasi 6
  • Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II (Beekeeping Officer Grade II) – Nafasi 21
  • Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II (Biomedical Engineer Grade II) – Nafasi 17
  • Fundi Sanifu Vifaa Tiba Daraja la II (Biomedical Engineering Technician Grade II) – Nafasi 34
  • Mhandisi Ujenzi Daraja la II (Civil Engineer Grade II) – Nafasi 53
  • Fundi Sanifu Msaidizi Ujenzi Daraja la II (Civil Technician Grade II) – Nafasi 48
  • Mpishi Daraja la II (Cook Grade II) – Nafasi 1,127
  • Katibu wa Kamati Daraja la II (Committee Clerk Grade II) – Nafasi 43
  • Afisa Maendeleo ya Jamii Daraja la II (Community Development Officer Grade II) – Nafasi 43
  • Mpishi Daraja la II (Cook II) – Nafasi 43
  • Afisa Ushirika Daraja la II (Cooperative Officer Grade II) – Nafasi 45
  • Afisa Mifugo Msaidizi Daraja la II (Livestock Field Officer Grade II) – Nafasi 252
  • Afisa Utamaduni Daraja la II (Cultural Officer Grade II) – Nafasi 38
  • Daktari wa Upasuaji wa Kinywa na Meno Daraja la II (Dental Surgeon Grade II) – Nafasi 68
  • Tabibu wa Kinywa na Meno Daraja la II (Dental Therapist Grade II) – Nafasi 217
  • Dereva Daraja la II (Driver Grade II) – Nafasi 427
  • Mchumi Daraja la II (Economist Grade II) – Nafasi 138
  • Afisa wa Sheria Daraja la II (Legal Officer Grade II) – Nafasi 140
  • Afisa Muuguzi Daraja la II (Nursing Officer Grade II) – Nafasi 712
  • Afisa Mifugo Daraja la II (Livestock Officer Grade II) – Nafasi 59
  • Afisa Mifugo Msaidizi Daraja la III (Livestock Field Officer Grade III) – Nafasi 15
  • Afisa Afya Mazingira Daraja la II (Environmental Health Officer Grade II) – Nafasi 96
  • Mhandisi Mazingira Daraja la II (Environmental Engineer Grade II) – Nafasi 4
  • Afisa Mazingira Daraja la II (Environmental Officer Grade II) – Nafasi 90
  • Afisa Uvuvi Daraja la II (Fisheries Officer Grade II) – Nafasi 55
  • Afisa Misitu Daraja la II (Forest Officer Grade II) – Nafasi 46
  • Fiziotherapia Daraja la II (Physiotherapist Grade II) – Nafasi 43
  • Afisa Wanyamapori Daraja la II (Game Officer Grade II) – Nafasi 32
  • Mhifadhi Wanyamapori Daraja la II (Game Warden Grade II) – Nafasi 16
  • Mhifadhi Wanyamapori Daraja la III (Game Warden Grade III) – Nafasi 2
  • Afisa Mipango Daraja la II (Planning Officer Grade II) – Nafasi 90
  • Afisa Michezo Daraja la II (Games and Sports Development Officer Grade II) – Nafasi 42
  • Mjiolojia Daraja la II (Geologist Grade II) – Nafasi 9
  • Msaidizi wa Afya Daraja la II (Health Assistant Grade II) – Nafasi 1,588
  • Afisa Teknolojia ya Maabara Daraja la II (Health Laboratory Scientist Grade II) – Nafasi 33
  • Katibu wa Afya Daraja la II (Health Secretary Grade II) – Nafasi 32
  • Afisa Rasilimali Watu Daraja la II (Human Resource Officer Grade II) – Nafasi 21
  • Afisa Habari Daraja la II (Information Officer Grade II) – Nafasi 84
  • Afisa Ukaguzi wa Ndani Daraja la II (Internal Audit Officer Grade II) – Nafasi 75
  • Mkaguzi wa Ndani Daraja la II (Internal Auditor Grade II) – Nafasi 102
  • Mtaalamu wa Maabara Daraja la II (Health Laboratory Technologist Grade II) – Nafasi 30
  • Dobi Daraja la II (Launderer Grade II) – Nafasi 10
  • Afisa Mipango Miji Daraja la II (Town Planner Grade II) – Nafasi 86
  • Fundi Sanifu Daraja la II (Mechanical Technician Grade II) – Nafasi 12
  • Daktari Daraja la II (Medical Officer Grade II) – Nafasi 1,201
  • Afisa Lishe Daraja la II (Nutrition Officer Grade II) – Nafasi 57
  • Mtoa Tiba kwa Vitendo Daraja la II (Occupational Therapist Grade II) – Nafasi 12
  • Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Office Management Secretary Grade II) – Nafasi 308
  • Mfamasia Daraja la II (Pharmacist Grade II) – Nafasi 138
  • Afisa Ununuzi Daraja la II (Procurement Officer Grade II) – Nafasi 114
  • Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (Records Management Assistant Grade II) – Nafasi 239
  • Afisa Kumbukumbu Daraja la II (Records Officer Grade II) – Nafasi 29
  • Fundi Sanifu Maabara ya Shule Daraja la II (School Laboratory Technician Grade II) – Nafasi 90
  • Afisa Ustawi wa Jamii Daraja la II (Social Welfare Officer Grade II) – Nafasi 148
  • Mtakwimu Daraja la II (Statistician Grade II) – Nafasi 100
  • Afisa Ugavi Daraja la II (Supplies Officer Grade II) – Nafasi 76
  • Afisa Utalii Daraja la II (Tourism Officer Grade II) – Nafasi 16
  • Afisa Biashara Daraja la II (Trade Officer Grade II) – Nafasi 164
  • Afisa Usafirishaji Daraja la II (Transport Officer Grade II) – Nafasi 51
  • Daktari wa Mifugo Daraja la II (Veterinary Officer Grade II) – Nafasi 36
  • Mtaalamu wa Dawa Daraja la II (Technologist Pharmacy Grade II) – Nafasi 130
  • Mwalimu Daraja la IIIA (Teacher Grade IIIA) – Nafasi 3,018

Sifa za Waombaji na Majukumu ya Kazi

Kwa mujibu wa tangazo hili, kila nafasi imeainishwa kwa majukumu na sifa maalum za kitaaluma. Miongoni mwao ni:

  • Mhasibu Daraja la II: Anatakiwa kuwa na Shahada ya Uhasibu au Stashahada ya Juu ya Uhasibu pamoja na cheti cha CPA(T) kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA).
  • Afisa Tawala Daraja la II: Shahada katika Utawala, Sayansi ya Siasa, Biashara au Utawala wa Umma.
  • Mhandisi Ujenzi Daraja la II: Shahada ya Uhandisi wa Ujenzi na usajili kutoka Bodi ya Wahandisi (ERB).
  • Afisa Mifugo Daraja la II: Shahada ya Sayansi ya Mifugo (Animal Science) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • Afisa Afya Mazingira: Shahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira pamoja na usajili kamili kutoka Bodi ya Wataalamu wa Afya ya Mazingira.
  • Afisa Uuguzi Msaidizi: Stashahada ya Uuguzi yenye usajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC).
  • Afisa Ununuzi Msaidizi: Stashahada ya Ununuzi na Ugavi, na awe amesajiliwa na Bodi ya PSPTB.
  • Afisa Ustawi wa Jamii: Stashahada au Shahada katika Social Work, Sociology, Psychology, au Child Protection.

Majukumu ya kazi yanajumuisha huduma kwa wananchi, usimamizi wa miradi ya maendeleo, utoaji wa huduma za afya, kilimo, uhasibu, pamoja na masuala ya utawala na maendeleo ya jamii.

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

Kwa mujibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, masharti ya jumla kwa waombaji wa ajira hizi ni kama ifuatavyo:

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45, isipokuwa wale walioko kazini Serikalini.
  2. Watu wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba, na kutaja aina ya ulemavu wao kwenye mfumo wa maombi.
  3. Waombaji waambatishe Wasifu Binafsi (CV) unaoonyesha anwani, simu na majina ya wadhamini watatu.
  4. Ni lazima kuambatisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria au wakili.
  5. Waajiriwa wa Serikali hawaruhusiwi kuomba ajira hizi.
  6. Vyeti vya kitaaluma vinavyohitajika ni pamoja na Postgraduate, Degree, Diploma, Certificates, na vyeti vya NECTA, NACTE au TCU kwa waliomaliza nje ya nchi.
  7. Testimonials, Provisional Results, au Statement of Results havitakubalika.
  8. Waombaji waliostaafu hawataruhusiwa kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  9. Taarifa za kughushi zitasababisha hatua za kisheria kuchukuliwa.

Jinsi ya Kutuma Maombi Kupitia Ajira Portal

Waombaji wote wanapaswa kutuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) unaopatikana kupitia tovuti rasmi: https://portal.ajira.go.tz

Barua ya maombi ya kazi inapaswa kuelekezwa kwa:

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
MTAA WA MAHAKAMA, TAMBUKARELI,
DODOMA, TANZANIA.

Mwisho wa Kutuma Maombi na Tahadhari Muhimu

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 29 Oktoba 2025.

Waombaji wote wanashauriwa kuhakikisha taarifa wanazowasilisha ni sahihi, kamili na zinazoambatana na vielelezo halisi.

Sekretarieti ya Ajira imeeleza kuwa zoezi hili ni la uwazi na linalolenga kutoa nafasi sawa kwa Watanzania wote wenye sifa. Kwa maelezo zaidi kuhusu Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025, tembelea tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira kupitia www.ajira.go.tz

Bofya Hapa Kupakua Pdf ya Tangazo Rasmi

Mada Zinazohusiana

Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs October 2025, ajira mpya serikalini 2025, ajira portal Tanzania, ajira za utumishi wa umma, nafasi za kazi serikali za mitaa, ajira mpya Wizara ya Afya, nafasi za walimu 2025, ajira mpya Tanzania.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili INEC 2025
  2. Posho na Malipo ya Wasimamizi wa Uchaguzi 2025
  3. Majina Ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Jimbo La Ubungo Na Kibamba
  4. Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Kigamboni
  5. Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam jimbo la Ukonga
  6. Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Segerea
  7. Majina Ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Jimbo La Lupembe
  8. Majina ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Jimbo la Ilala
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo