Nafasi Mpya Za Kazi MDAs NA LGAs Agosti 2024 (Ajira Mpya MDAs NA LGAs)
Serikali ya Tanzania, kupitia Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, imetangaza nafasi mpya za kazi zaidi ya 6,000 katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs). Hii ni fursa ya kipekee kwa Watanzania wenye sifa na ujuzi kujiendeleza kitaaluma na kuchangia katika maendeleo ya taifa.
Nafasi za Kzi Zilizotangazwa MDAs NA LGAs Agosti 2024
Tangazo la ajira mpya MDAs NA LGAs Agosti 2024 linajumuisha nafasi mbalimbali za kazi katika sekta mbalimbali, ikiwemo:
- Msaidizi wa Ufugaji Nyuki Daraja la II (Beekeeping Assistant II) – Nafasi 47
- Mpima Ardhi Daraja la II (Land Surveyor II) – Nafasi 4
- Afisa Ununuzi Daraja la II (Procurement Officer II) – Nafasi 350
- Afisa Uvuvi Daraja la II (Fisheries Officer II) – Nafasi 90
- Dereva Daraja la II (Driver II) – Nafasi 514
- Afisa Wanyamapori Daraja la II (Game Officer II) – Nafasi 26
- Afisa Misitu Daraja la II (Forest Officer II) – Nafasi 91
- Afisa Mazingira Daraja la II (Environmental Officer II) – Nafasi 119
- Afisa Usafirishaji Daraja la II (Transport Officer II) – Nafasi 56
- Afisa Utalii Daraja la II (Tourism Officer II) – Nafasi 27
- Afisa Ushirika Daraja la II (Cooperative Officer Grade II) – Nafasi 27
- Afisa Kilimo Daraja la II (Agricultural Officer II) – Nafasi 105
- Afisa Kilimo Msaidizi Daraja la II (Agricultural Field Officer II) – Nafasi 481
- Afisa Kilimo Msaidizi Daraja la III (Agricultural Field Officer III) – Nafasi 477
- Afisa Habari Daraja la II (Information Officer II) – Nafasi 63
- Afisa Ununuzi Msaidizi Daraja la II (Assistant Procurement Officer II) – Nafasi 120
- Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (Records Management Assistant II) – Nafasi 382
- Mpishi Daraja la Pili (Cook II) – Nafasi 78
- Mhasibu Daraja la II (Accountant II) – Nafasi 350
- Afisa Utamaduni Daraja la II (Cultural Officer II) – Nafasi 6
- Afisa Utamaduni Msaidizi Daraja la II (Assistant Cultural Officer II) – Nafasi 6
- Mhifadhi wa Wanyamapori Daraja la III (Game Warden III) – Nafasi 6
- Afisa Michezo Daraja la II (Game and Sports Development Officer II) – Nafasi 29
- Afisa Utumishi Daraja la II (Human Resource Officer II) – Nafasi 95
- Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II (Beekeeping Officer II) – Nafasi 32
- Afisa Uvuvi Msaidizi Daraja la II (Assistant Fisheries Officer II) – Nafasi 87
- Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Office Management Secretary II) – Nafasi 350
- Msaidizi wa Mifugo Daraja la II (Livestock Field Assistant II) – Nafasi 182
- Mchumi Daraja la II (Economist II) – Nafasi 138
- Mtakwimu Daraja la II (Statistician II) – Nafasi 128
- Afisa TEHAMA Msaidizi Daraja la II (Assistant Information and Communication Technology Officer II) – Nafasi 64
- Afisa Biashara Daraja la II (Trade Officer II) – Nafasi 193
- Mhandisi Ujenzi Daraja la II (Civil Engineer II) – Nafasi 85
- Msanifu Majengo Daraja la II (Architect II) – Nafasi 63
- Afisa Hesabu Daraja la II (Accounts Officer II) – Nafasi 380
- Msaidizi wa Hesabu Daraja la II (Accounts Assistant II) – Nafasi 200
- Mhandisi Kilimo Daraja la II (Agro Engineer II) – Nafasi 30
- Afisa Ustawi wa Jamii Msaidizi Daraja la II (Assistant Social Welfare Officer II) – Nafasi 229
- Msaidizi wa Hesabu Daraja la I (Accounts Assistant I) – Nafasi 150
- Afisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi Daraja la II (Assistant Community Development Officer II) – Nafasi 327
- Fundi Sanifu Daraja la II – Kilimo (Agricultural Technician II) – Nafasi 40
- Mkadiriaji Majenzi Daraja la II (Quantity Surveyor II) – Nafasi 30
Sifa za Waombaji Nafasi Mpya Za Kazi MDAs NA LGAs
Kwa waombaji wanaotaka kuomba nafasi hizi, wanashauriwa kuwa na sifa na uwezo unaotakiwa kwa nafasi husika. Sifa za waombaji zinatofautiana kulingana na nafasi husika. Vigezo na masharti ya kila nafasi yameainishwa katika tangazo la ajira ambalo linapatikana kwenye tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Lakini kwa ujumla, waombaji wanatakiwa kuwa:
- Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa kwa watumishi waliopo serikalini).
- Wenye elimu na ujuzi unaotakiwa kwa nafasi husika, kuanzia kidato cha nne hadi shahada ya kwanza.
- Wenye uadilifu na bidii katika kazi.
Jinsi ya Kutuma Maombi Ajira Mpya MDAs NA LGAs
Maombi yote ya nafasi hizi mpya za ajira 6,257 zilizotangazwa MDAs NA LGAs Agosti 2024 yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: http://portal.ajira.go.tz.
Waombaji wanapaswa kuambatisha nyaraka zote muhimu, ikiwa ni pamoja na CV, vyeti vya elimu, na barua ya maombi. Pia waombaji wanapaswa kuambatisha barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
- KATIBU,
- OFISI YA RAIS,
- SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
- S. L. P. 2320, DODOMA.
Masharti Ya Jumla Kwa Waombaji wa Nafasi za Kazi MDAs NA LGAs Agosti 2024
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali na vyeti vya kitaaluma kulingana na sifa husika kama ifuatavyo;.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Cheti cha kuzaliwa
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi Kazi MDAs NA LGAs ni tarehe 16 Agosti, 2024.
Mapendekezo ya Mhariri:
Kazi nzuri
Mfumo huu ni rafiki kwa watumiaji wote, naomba watanzania tuutumie
Very good kwa viongozi wa Secretariat ya utumishi
Kaz nzuri