NECTA Yatangaza Usajili wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE na FTNA 2026

NECTA Yatangaza Usajili wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE na FTNA 2026

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi kufunguliwa kwa dirisha la usajili kwa watahiniwa wa kujitegemea wanaotarajia kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) pamoja na Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) kwa mwaka 2026. Tangazo hili linawahusu watahiniwa wote ambao hawajasajiliwa kupitia shule au taasisi, bali wanajisajili binafsi kwa mujibu wa taratibu za NECTA.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, NECTA imeweka wazi ratiba ya usajili, viwango vya ada, pamoja na maelekezo muhimu ambayo kila mtahiniwa wa kujitegemea anatakiwa kuyafuata ili kukamilisha usajili wake kwa usahihi ndani ya muda uliopangwa.

Tarehe Rasmi za Usajili kwa Watahiniwa wa Kujitegemea 2026

NECTA imeeleza kuwa usajili wa watahiniwa wa kujitegemea kwa mitihani ya CSEE na FTNA umeanza rasmi tarehe 01 Januari 2026 na utaendelea hadi tarehe 28 Februari 2026. Kipindi hiki ndicho kinachotambulika kama usajili wa kawaida.

Kwa watahiniwa watakaochelewa kujisajili, NECTA imeruhusu dirisha la ziada kuanzia tarehe 01 Machi 2026 hadi 31 Machi 2026, ambapo ada ya usajili itaongezwa kutokana na faini ya kuchelewa.

Ada za Usajili CSEE na FTNA 2026

Katika kipindi cha usajili wa kawaida, ada zilizopangwa ni kama ifuatavyo:

  • Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE): Shilingi 50,000/=
  • Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA): Shilingi 10,000/=

Kwa watahiniwa watakaosajiliwa kwa kuchelewa, kuanzia Machi 2026, ada zitakuwa:

  • CSEE: Shilingi 65,000/= (ikiwemo ada pamoja na faini)
  • FTNA: Shilingi 15,000/= (ikiwemo ada pamoja na faini)

NECTA imesisitiza umuhimu wa kuzingatia ratiba ya usajili ili kuepuka gharama za ziada.

Hatua Muhimu Kabla ya Usajili Mtandaoni

Kabla ya mtahiniwa wa kujitegemea kusajiliwa rasmi kwenye mfumo wa usajili wa NECTA, anatakiwa kufuata utaratibu maalum. Kwanza, mwombaji anatakiwa kwenda kwenye Kituo cha Mitihani anachokusudia kufanya mtihani ili kuchukua namba rejea (reference number). Namba hizi hutolewa bure na zinahitajika kwa hatua zinazofuata za usajili.

Baada ya kupata namba rejea, mtahiniwa anatakiwa kufanya malipo ya ada ya usajili kupitia Benki, kwa kutumia Control Number itakayohusishwa na namba hiyo ya rejea.

Utaratibu wa Kutengeneza Control Number na Kujisajili

NECTA imeeleza kuwa maelezo ya kina kuhusu hatua za kutengeneza Control Number na namna ya kukamilisha usajili mtandaoni yatatolewa na Mkuu wa Kituo cha Mtihani ambacho mtahiniwa amekichagua. Hivyo, watahiniwa wanashauriwa kushirikiana kwa karibu na wakuu wa vituo husika ili kuhakikisha usajili wao unafanyika kwa usahihi.

NECTA Yatangaza Usajili wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE na FTNA 2026

Bofa Hapa Kupakua Tangazo Rasmi Kuhusu Usajili wa Watahiniwa Binafsi

Mapednekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Darasa la Nne 2025 (NECTA Standard Four Results)
  2. Matokeo ya Darasa la Nne 2025/2026 (NECTA SFNA Results)
  3. Fomu za Kujiunga Vyuo Vya VETA 2026
  4. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo vya VETA 2026
  5. Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo