Novatus Miroshi Ajiunga na Goztepe ya Uturuki
Klabu ya Goztepe ya Uturuki imethibitisha kumsajili Novatus Dismas Miroshi, nyota mchanga wa soka kutoka Tanzania kwa mkataba wa miaka minne. Hatua hii muhimu inamweka Novatus katika nafasi ya kukua zaidi katika ulimwengu wa soka la kulipwa la kimataifa, baada ya kuwa na msimu mzuri akiwa kwa mkopo na katika klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Safari ya Soka ya Novatus Dismas Miroshi
Novatus, mwenye umri wa miaka 21, amekuwa akionyesha uwezo wake mkubwa katika soka la Ulaya na pale anapukua katika timu ya taifa ya Tanzania Taifa Star. Kabla ya kujiunga na klabu ya Goztepe, alikuwa akiichezea Shakhtar Donetsk kwa mkopo kutoka Zulte Waregem ya Ubelgiji. Katika msimu wake na Shakhtar Donetsk, Novatus alishiriki katika Ligi Kuu ya Ukraine na hata kufikia hatua ya UEFA Champions League, ambapo alionyesha ustadi wake mkubwa katika uwanja wa kimataifa.
Uhamisho wa Novatus kwenda Goztepe ni hatua muhimu sana katika kazi yake ya soka. Kucheza katika ligi ya Uturuki kunamweka katika mazingira mapya ya kitamaduni na kimichezo, na kumwezesha kukuza ujuzi wake katika soka la kimataifa. Mkataba wake wa miaka minne unaonesha imani ya timu na uwezo wake, na tunaweza kutarajia Novatus kuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio ya Goztepe.
Taarifa Kuhusu Goztepe katika Ligi Kuu ya Uturuki
Goztepe ni moja kati ya timu zinazokua kwa kasi katika soka la Uturuki. Timu hii imeweza kupanda daraja na kujitengenezea nafasi ya kushiriki Ligi Kuu ya Uturuki kuanzia msimu wa 2024/25, baada ya kumaliza nafasi ya pili katika ligi daraja la kwanza. Uwezo wa Novatus utachangia pakubwa kuimarisha safu ya kati ya Goztepe, huku timu ikilenga kufanya vizuri katika mashindano ya ndani na kimataifa.
Mapendekezo ya mhariri:
- Awesu na Onana Watua Misri Kujiunga na Kambi ya Mazoezi ya Simba
- Vilabu Bora Afrika 2023/2024 (IFFHS Club Ranking)
- Washindi wa Tuzo Dar Port Kagame Cup 2024, Hawa Apa
- Bingwa wa Dar Port Kagame Cup 2024 ni Red Arrows
- APR Yatangulia Fainali Cecafa Dar Port Kagame Cup 2024
- Azam Fc Yasajili Kiungo Mkabaji Kutoka CR Belouizdad
- Wachezaji Waliosajiliwa Simba 2024/2025
- Wachezaji Wapya Yanga | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
Weka Komenti