Orodha ya Mabingwa wa Kombe La Shirikisho Tanzania (Mabingwa wa Kombe La FA Tanzania)
Kombe la Shirikisho la Tanzania au Kombe la FA, lililokua maarufu kama Azam Sports Federation Cup kutokana na udhamini kabla ya CRDB bank kutangazwa kuwa mdamini mpya katika msimu wa 2023/2024 na kupewa jina la CRDB bank federation Cup, ni moja kati ya michuano soka nchini Tanzania yenye ushindani mkubwa na kufuatiliwa na mashabiki wengi baada ya Ligi kuu Tanzania bara.
Kombe la shirikisho huleta pamoja timu kutoka ligi mbalimbali nchini kushiriki katika mchuano wa kusisimua. Tangu kuanzishwa kwake, Kombe la Shirikisho limekuwa jukwaa muhimu kwa vilabu kujipatia umaarufu na fursa ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Mashindano haya yamekuwa na mabadiliko kadhaa katika muundo na jina lake kwa miaka mingi, lakini msisimko na ushindani wake umebaki kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka nchini. Kila mwaka, timu hujitahidi kupata nafasi ya kuingia kwenye vitabu vya historia kwa kunyakua taji la Kombe la Shirikisho. Katika chapisho hili, tutazama kwa undani historia ya Kombe la Shirikisho, orodha kamili ya mabingwa na jinsi mabingwa hao walivyo beba ushindi.
Orodha ya Mabingwa wa Kombe La Shirikisho Tanzania
Jedwali lifuatalo linaonyesha orodha kamili ya mabingwa wa Kombe la Shirikisho (Kombe la FA) la Tanzania, kuanzia ilipoanzishwa kama FAT Cup (Bara) hadi sasa hivi ikiwa inafahamika kama CRDB Bank Federation Cup:
Mwaka | Bingwa | Mshindi wa pili | Matokeo Fainali |
Zama za FAT Cup (Bara) | |||
1967 | Young African FC (Dar-es-Salaam) | Liverpool | 2-0 |
1974 | Young African FC (Dar-es-Salaam) | Simba SC (Dar-es-Salaam) | 2-1 (aet) |
1985 | Maji Maji (Songea) | ||
1995 | Simba SC (Dar-es-Salaam) | ||
1996 | Sigara | Young African FC (Dar-es-Salaam) | bt |
1997 | Tanzania Stars (Dar-es-Salaam) | ||
1998 | Tanzania Stars (Dar-es-Salaam) | Simba SC (Dar-es-Salaam) | 2-0 |
1999 | Young African FC (Dar-es-Salaam) | ||
2000 | Mtibwa Sugar | Simba SC (Dar-es-Salaam) | 1-0 |
2001 | Young African FC (Dar-es-Salaam) | Moro United (Morogoro) | 2-0 |
2002 | JKT Ruvu Stars (Coast Region) | Baker Rangers (Manzese) | bt |
2003-2015 | Hakikufanyika | ||
Zama za Azam Sports Federation Cup | |||
2015/16 | Young African FC (Dar-es-Salaam) | Azam FC (Dar-es-Salaam) | 3-1 |
2016/17 | Simba SC (Dar-es-Salaam) | Mbao (Mwanza) | 2-1 (aet) |
2017/18 | Mtibwa Sugar | Singida United | 3-2 |
2018/19 | Azam FC (Dar-es-Salaam) | Lipuli FC (Iringa) | 1-0 |
2019/20 | Simba SC (Dar-es-Salaam) | Namungo FC (Lindi) | 2-1 |
2020/21 | Simba SC (Dar-es-Salaam) | Young African FC (Dar-es-Salaam) | 1-0 |
2021/22 | Young African FC (Dar-es-Salaam) | Coastal Union FC (Tanga) | 3-3 (aet, 4-1 pen) |
2022/23 | Young African FC (Dar-es-Salaam) | Azam FC (Dar-es-Salaam) | 1-0 |
Zama za CRDB Bank Federation Cup | |||
2023/24 | Young African FC (Dar-es-Salaam) | Azam FC (Dar-es-Salaam) | 0-0 (aet, 6-5 pen) |
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Picha Za Parade ya Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24
- Orodha Ya Mabingwa Wa UEFA Champions League
- Wachezaji Wapya Yanga | Wachezaji Waliosajiliwa Yanga 2024/2025
- Timu zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Euro 2024
- Orodha Ya Wafungaji Bora Ligi Kuu Ya NBC Tanzania 2023/2024
- Orodha Ya Washindi Wa Ligi Kuu Ya Uingereza Miaka Yote
- Orodha Kamili ya Makombe na Tuzo za Toni Kroos
Weka Komenti