Orodha ya Matajiri Tanzania 2024 | List ya Matajiri Tanzania forbes 2024
Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi na vivutio vingi vya utalii. Tanzania ni yapili kwa ukubwa katika Afrika mashariki na kutokana na rasilimali na fursa mbalimbali zilizopo nchini, kuna baadhi ya watanzania wameweza kutumia busara na ubunifu wao kujipatia kipato kikubwa ambacho kimewafanya wajijengee heshima kubwa kutokana na utajiri walioupata.
Matajiri wa Tanzania wengi wamejipatia utajiri wao kupitia shughuli mbalimbali za kibiashara kama vili kumiliki viwanda vya uzalishazi wa bidhaa mbalimbali za chakula na vinywaji, Kulima mazao mbalimbali ya biashara na hata utoaji wa huduma za kijamii. Katika chapisho hili Tumekuletea Orodha ya Matajiri Tanzania 2024 kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa na Forbes.
Orodha ya Matajiri Tanzania 2024
- Mohammed Dewji
- Rostam Azizi
- Said Salim Bakhresa
- Reginald Mengi
- Ally Awadh
- Shekhar Kanabar
- Shubash Patel
- Fida Hussein Rashid
- Salim Turkey
- Ghalib Said Mohammed
- Yogesh Manek
Tajiri Wa Kwanza Tanzania 2024: Mohammed Dewji ($1.8B kwa Taarifa ya 7/3/24)
Mohammed Dewji ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa Afrika mashariki na miongoni watu matajiri zaidi nchini Tanzania kulingana na taarifa za hivi karibuni zilizotolewa na Forbes. Akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.8 kwa mujibu wa taarifa ya tarehe 3 Julai 2024, Dewji ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa na wenye mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania.
Kuhusu Utajiri wa Mohammed Dewji
Mohammed Dewji ni Mkurugenzi Mtendaji wa METL, kongomolate la Kitanzania lililoanzishwa na baba yake katika miaka ya 1970. METL inajihusisha na uzalishaji wa nguo, usagaji wa unga, vinywaji, na mafuta ya kula katika maeneo ya Afrika Mashariki, Kusini na Kati.
Pamoja na Tanzania, METL inaendesha shughuli zake katika nchi 10 za Afrika ikiwemo Uganda, Ethiopia, na Kenya. Mohammed Dewji ndiye bilionea pekee wa Tanzania na alitia sahihi kwenye Ahadi ya Kutoa (Giving Pledge) mwaka 2016, akiahidi kutoa angalau nusu ya utajiri wake kwa shughuli za kijamii.
Takwimu Binafsi
- Umri: 49
- Chanzo cha Utajiri: Kimegawanyika
- Mahali alipoishi: Dar es Salaam, Tanzania
- Uraia: Mtanzania
- Hali ya Mahusiano: Ameoa
- Watoto: 3
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti