Ratiba Ya Kombe La Mapinduzi 2026 (Mapinduzi CUP 2026)

Ratiba Ya Kombe La Mapinduzi 2026 (Mapinduzi CUP 2026)

Michuano ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi Desemba 28, 2025, ambapo klabu ya Mlandege itapambana na Singida Black Stars katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo.

Mashindano haya ya kihistoria yatafanyika Zanzibar, yakihusisha timu kumi kutoka Tanzania Bara, Zanzibar pamoja na mgeni kutoka Uganda, yakilenga kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar huku yakitoa burudani ya kiwango cha juu kwa mashabiki wa soka.

Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2026 imewekwa hadharani na Kamati ya Kombe la Mapinduzi, ikionyesha mpangilio kamili wa michezo kuanzia hatua ya makundi hadi fainali itakayochezwa Januari 13, 2026.

Ufunguzi wa Mashindano na Uwanja Utakaotumika

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi 2026, Rashid Said Suleiman, mchezo wa ufunguzi kati ya Mlandege na Singida Black Stars utachezwa Desemba 28, 2025 saa 10:15 jioni katika Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja. Siku hiyo hiyo, kutakuwa na mchezo mwingine wa kuvutia kati ya Azam FC na URA ya Uganda, utakaopigwa saa 2:15 usiku katika uwanja huo huo.

Akizungumza kuhusu mpangilio wa mashindano, Suleiman alisema:

“Kwa sababu mara ya mwisho kumalizia kwa namna hii ya klabu kabla ya iliyopita kushirikisha timu za taifa, bingwa alikuwa Mlandege, hivyo tunawachukulia kama bingwa mtetezi wa mashindano haya.”

Aliongeza kuwa:

“Kwa maana hiyo, yeye ndiye atafungua mashindano yetu kwa siku hiyo kukutana na timu ya Singida. Siku hiyohiyo, usiku wake tutakuwa na mechi kati ya Azam na URA.”

Hatua zote za makundi pamoja na nusu fainali zitachezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, huku fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026 ikipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Gombani uliopo Pemba, Januari 13, 2026.

Ratiba Kamili ya Kombe la Mapinduzi 2026

Tarehe Muda Mchezo
Desemba 28, 2025 10:15 jioni Mlandege vs Singida Black Stars
2:15 usiku Azam vs URA
Desemba 29, 2025 10:15 jioni Fufuni vs Mwembe Makumbi
2:15 usiku KVZ vs TRA United
Desemba 31, 2025 10:15 usiku Mlandege vs URA
2:15 usiku Singida Black Stars vs Azam
Januari 2, 2026 2:15 usiku Azam vs Mlandege
Januari 3, 2026 10:15 jioni Singida Black Stars vs URA
2:15 usiku Simba vs Mwembe Makumbi
Januari 4, 2026 2:15 usiku Yanga vs KVZ
Januari 5, 2026 2:15 usiku Fufuni vs Simba
Januari 6, 2026 2:15 usiku Yanga vs TRA United
Januari 8, 2026 2:15 usiku Nusu Fainali ya Kwanza
Januari 9, 2026 2:15 usiku Nusu Fainali ya Pili
Januari 13, 2026 2:15 usiku Fainali

Ratiba Ya Kombe La Mapinduzi 2026 (Mapinduzi CUP 2026)

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za Taifa Stars AFCON 2025
  2. Taifa Stars Tayari kwa AFCON 2025 Baada ya Kuwasili Morocco
  3. CV Ya Steve Barker Kocha Mpya wa Simba 2025/2026
  4. Bei ya Tiketi za Kombe la Dunia 2026 Yazua Mjadala Mkubwa Duniani
  5. Mchango Mkubwa wa Salah Waipa Liverpool Ushindi Mnono Dhidi ya Brighton
  6. Timu Nane Zathibitishwa Kushiriki Kombe la Mapinduzi 2026 Zanzibar
  7. Ratiba Ya AFCON 2025 Hatua Ya Makundi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo