Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 10/04/2026
Michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB inaendelea kutimua vumbi leo Ijumaa, Aprili 10, 2026, huku hatua ya 16 bora ikiingia katika mzunguko mwingine muhimu wa ushindani. Timu nne zitakuwa dimbani kuwania nafasi ya kusonga mbele, katika michezo miwili itakayochezwa kwa wakati mmoja kuanzia saa 10:00 jioni.
Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup leo inaonesha wazi mechi zitakazochezwa, zikihusisha timu zenye malengo ya kufika hatua za juu za mashindano haya ya mtoano:
JKT Tanzania vs Mbuni FC
- Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam
- Saa 10:00 jioni
Geita Gold vs Mashujaa FC
- Uwanja wa Shule ya Wasichana Nyankumbu, Geita
- Saa 10:00 jioni
Mchezo kati ya Geita Gold na Mashujaa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia ya timu hizi kila zinapokutana. Kocha wa Mashujaa, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, alielezea uzito wa pambano hilo akisisitiza kuwa si mchezo wa kawaida bali ni vita ya ushindani wa hali ya juu.
“Ukiangalia Geita Gold kwenye Championship, ukikutana nayo utakuja kufedheheka mtu mzima, kwahiyo tunaingia kucheza na watu wazima wenzetu ambao walikuwa kwenye Ligi Kuu, sio mechi ya kitoto lakini tumejipanga kupambana kama ambavyo wenzetu wamejipanga ili mwenye bahati na aliyejipanga vizuri aweze kusonga mbele,” amesema Julio.
Julio aliongeza kuwa licha ya ugumu wa mashindano hayo, kikosi chake kimejipanga kuhakikisha kinapata matokeo chanya, kikilenga kusonga mbele huku pia kikijenga msingi wa kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya ndani na malengo ya kucheza kimataifa msimu ujao.
Kwa upande wa Geita Gold, kocha Zuberi Katwila alifafanua mkakati wa kutumia kikosi mseto, akiwapa nafasi wachezaji ambao hawapati muda mwingi kwenye ligi. Alieleza kuwa mfumo huo wa mzunguko wa wachezaji umekuwa sehemu ya mafanikio ya timu kufika hatua hii.
“Ni ‘rotation’ ambayo tulikuwa tunaifanya toka awali, wanaocheza Championship ni wengine na watakaocheza FA ni wengine, mechi zetu zote za FA wanatumika hao ambao ni wachezaji wetu lakini katika Championship wanakuwa kidogo wanakosa nafasi, hii ni mtoano ambayo lazima utumie wachezaji ambao watakuwa na nguvu ya kutosha kupambana na mchezo,” amesema Katwila.
Katika hatua nyingine, mashabiki watakaofika kushuhudia mchezo wa Geita Gold dhidi ya Mashujaa watapata fursa ya kipekee kuingia bure, baada ya tiketi zote kulipiwa na mlezi wa klabu hiyo, Yefred Myenzi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
- Matokeo ya Pamba Jiji vs Yanga Leo 08/04/2026
- Harry Maguire Asaini Mkataba Mpya Manchester United Hadi 2027
- AFCON 2027 Kufanyika Mwezi Juni na Julai
- Droo ya Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza: Man City Yapangwa na Southampton, Chelsea Uso kwa Uso Dhidi ya Leeds
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali FA Cup Pemba







Leave a Reply