Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/04/2026
Michuano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara inaendelea leo, Alhamisi Aprili 9, 2026, huku mechi mbili muhimu zikitarajiwa kuchezwa katika mikoa ya Arusha na Manyara. Ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/04/2026 inaleta ushindani mkali unaohusisha Simba SC, TRA United, Azam FC na Mbeya City, kila timu ikiwa na malengo mahsusi ya kupata matokeo chanya.
Mechi za Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/04/2026
TRA United vs Simba SC
- Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
- Muda; 4:00 pm
Mbeya City vs Azam FC
- Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara
- Muda; 4:00 pm
Ndani ya dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Simba itakuwa mgeni wa TRA United katika mchezo wa kiporo uliosogezwa mbele kutokana na mvua kubwa zilizonyesha awali. Mchezo huu unakuja wakati Simba ikitafuta kurejea kwenye ushindi baada ya kuangusha pointi mbili mbele ya Azam, huku TRA United ikisaka matokeo ya kuvunja rekodi mbaya dhidi ya wapinzani hao.
Rekodi zinaonyesha kuwa Simba imekuwa na ubora mkubwa katika mikutano yao iliyopita. Katika mechi tano walizokutana, Simba imeshinda zote na kufunga mabao 15, huku TRA United ikiwa haijawahi kufunga bao lolote dhidi yao. Hata hivyo, Simba imekuwa na changamoto kwenye mechi za ugenini, ambapo katika mechi tano zilizopita imeshinda mbili na kutoa sare tatu.
Kocha wa Simba, Steve Barker, amesema wanatarajia mchezo mgumu lakini wamejipanga kupata ushindi. Kwa upande wa TRA United, kocha Ettiene Ndayiragije ameielezea Simba kama timu yenye ubora mkubwa lakini akaeleza kuwa watajaribu kuzuia nguvu zao na kutumia makosa yao kupata matokeo.
TRA United ina rekodi nzuri ya nyumbani ikiwa imeshinda mechi tatu kati ya tano, lakini itaikosa huduma ya Chamou Karaboue na Mzamiru Yassin kutokana na masharti ya mikataba yao ya mkopo.
Katika mchezo mwingine, Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Azam FC kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mkoani Manyara. Huu ni mchezo unaozikutanisha timu zenye historia tofauti, huku Azam ikiwa na rekodi bora katika mikutano yao.
Katika mechi 18 zilizopita, Azam imeshinda 13, Mbeya City ikishinda moja na sare nne. Azam pia imefunga mabao 29 dhidi ya mabao tisa ya Mbeya City. Licha ya ubora huo, Azam imekuwa na changamoto kwenye mechi za ugenini, ikishinda mbili na kutoa sare tatu katika michezo mitano iliyopita.
Mbeya City inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na morali baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya KMC, matokeo ambayo yanaongeza nguvu kwa kikosi hicho kuelekea mchezo wa leo.
Kwa ujumla, ratiba ya Ligi Kuu Ya NBC Leo 09/04/2026 inaleta mechi zenye ushindani mkubwa, ambapo kila timu inalenga kupata matokeo yatakayosaidia nafasi zao kwenye msimamo wa ligi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
- Matokeo ya Pamba Jiji vs Yanga Leo 08/04/2026
- Harry Maguire Asaini Mkataba Mpya Manchester United Hadi 2027
- AFCON 2027 Kufanyika Mwezi Juni na Julai
- Droo ya Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza: Man City Yapangwa na Southampton, Chelsea Uso kwa Uso Dhidi ya Leeds
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali FA Cup Pemba









Leave a Reply