Ratiba ya Mechi za Leo 14/08/2025 CHAN
Michuano ya African Nations Championship (CHAN) 2024, inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani pekee barani Afrika, inaendelea leo Alhamisi, Agosti 14, 2025 katika viwanja mbalimbali vya Afrika Mashariki. Mashindano haya yanachezwa kwa mfumo wa ushirikiano wa mataifa matatu Kenya, Tanzania na Uganda na yamekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa kandanda kote barani.
Leo, mashabiki wa soka wanatarajia burudani ya kiwango cha juu kupitia michezo miwili mikali ya hatua ya makundi. Kwa mujibu wa Ratiba ya Mechi za Leo 14/08/2025 CHAN, viwanja vya Nyayo na Kasarani vitashuhudia pambano kali, huku kila timu ikisaka pointi muhimu za kusonga mbele. Mechi zote zitakuwa mubashara kupitia chaneli mbalimbali za michezo ikiwemo Azam Max na Azam Sports.
1. Morocco vs Zambia – Saa 11:00 Jioni (Nyayo Stadium, Kenya)
Hii ni nafasi nyingine kwa Morocco kujiuliza kilichowakumba walipofungwa na Kenya katika mchezo uliopita. Timu hiyo inaingia dimbani leo ikiwania ushindi wa pili katika mchezo wao wa tatu, ili kuweka hai matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata.
Kwa upande mwingine, Zambia hawana budi kupambana kwa nguvu zote. Baada ya kupoteza mechi zao mbili za mwanzo, wanahitaji angalau alama moja ili wasiondoke mikono mitupu kwenye michuano hii ya CHAN 2024. Hii itakuwa mechi ya presha kubwa kwa pande zote mbili, na mashabiki wanategemea kushuhudia upinzani mkali kuanzia dakika ya kwanza.
2. Angola vs DR Congo – Saa 2:00 Usiku (Kasarani Stadium, Kenya)
Pambano hili linaweza kufananishwa na fainali ndogo kwa sababu ya umuhimu wake. DR Congo wanapigania nafasi ya kusalia kwenye mashindano, baada ya kukumbana na matokeo yasiyoridhisha kwenye mechi zilizopita. Ushindi ndio tiketi yao pekee ya kusonga mbele.
Kwa upande wa Angola, hii ni mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi, na watakuwa wanapigania heshima na nafasi ya kumaliza kwa alama za juu. Uwanja wa Kasarani unatarajiwa kujaa kelele na nderemo za mashabiki, huku dakika 90 zikiahidi kuwa za msisimko mkubwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ifahamu Gaborone United Wapinzani wa Simba Ligi ya Mabingwa CAF 2025/2026
- Makundi ya CHAN 2025 Yatangazwa
- Ifahamu Wiliete Benguela Wapinzani wa Yanga CAF 2025/2026
- Simba Yatangaza Bei ya Jezi Zao Mpya za 2025-2026
- Msimamo wa Makundi CHAN 2025
- Ratiba ya Mechi za Leo 12/08/2025 CHAN
- Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/2026
Leave a Reply