Ratiba ya Mechi za Leo 22/09/2025
Leo Jumatatu ya tarehe 22/09/2025, mashabiki wa soka duniani wataweza kushuhudia mitanange mikali kutoka katika ligi mbalimbali barani Ulaya na Afrika. Michezo hii imepangwa kuchezwa katika viwanja tofauti huku kivutio kikubwa kikiwa ni mechi za Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Serie A Italia, Ligue 1 Ufaransa, na Primeira Liga ya Ureno. Ratiba hii ni muhimu kwa mashabiki na wadau wa michezo ili kujua muda na mechi zitakazochezwa leo.
Ratiba ya Mechi za Leo 22/09/2025
Ligi Kuu ya NBC Tanzania
19:00 Coastal Union vs JKT Tanzania
Mtanange huu wa ligi ya ndani unatarajiwa kuvutia mashabiki wengi, kwani timu zote mbili zinawania nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi. Coastal Union itakuwa na faida ya kucheza nyumbani, lakini JKT Tanzania ni wapinzani wenye ushindani mkubwa.
France Ligue 1
21:00 Marseille vs PSG
Mechi hii ni miongoni mwa michezo mikubwa zaidi leo. Marseille na Paris Saint-Germain (PSG) zimekuwa na upinzani wa muda mrefu katika ligi ya Ufaransa, na mara zote pambano hili huchukuliwa kama “Classique ya Ufaransa.” Mashabiki wanatarajia mchezo wenye ushindani wa hali ya juu na nyota kadhaa uwanjani.
Italy Serie A
21:45 Napoli vs Pisa
Katika Serie A, mabingwa wa zamani Napoli watakuwa wenyeji wa Pisa. Hii ni nafasi ya Napoli kuendeleza ubabe wao, lakini Pisa inaweza kutoa upinzani wa kushtukiza. Mashabiki wa Serie A bila shaka watakuwa na hamu ya kuona matokeo ya mchezo huu.
Portugal Primeira Liga
22:15 Sporting vs Moreirense
Usiku huu, macho pia yataelekezwa nchini Ureno ambapo Sporting Lisbon watavaana na Moreirense. Sporting, moja ya klabu kongwe na zenye mafanikio nchini humo, inatarajiwa kutumia mchezo huu kujiimarisha zaidi katika mbio za ubingwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya Gaborone United vs Simba leo 20/09/2025
- Hiki Apa Kikosi cha Simba vs Gaborone United leo 20/09/2025
- Viwango Vya FIFA Duniani 2025 (FIFA Rankings)
- Taifa Stars Yashuka Nafasi Nne Katika Orodha Mpya ya Viwango vya FIFA
- Benfica Yampa Mourinho Kibarua cha Kuiongoza kwa Miaka Miwili
- Yanga Yaanza Msimu wa Ligi ya Mabingwa Kwa Ushindi wa 3-0
- TRA Yaingia Rasmi Kwenye Michezo Baada ya Kuinunua Tabora United
- Matokeo Wiliete Sc vs Yanga Leo 19/09/2025
Leave a Reply