Ratiba ya Mechi za Leo 24/09/2025

Ratiba ya Mechi za Leo 24/09/2025

Mashabiki wa soka kote duniani wanatarajia burudani kubwa leo Jumatano, tarehe 24 Septemba 2025, ambapo kutakuwa na mitanange kadhaa ya kukatana shoka kutoka ligi kuu za ndani, michuano ya kimataifa ya Ulaya, pamoja na hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Ratiba ya mechi hizi ni sehemu muhimu kwa wapenzi wa kandanda kufuatilia timu zao pendwa na matokeo yanayoweza kuamua mwenendo wa msimu huu.

Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania

Kwa upande wa soka la nyumbani, leo mashabiki watashuhudia michezo mikubwa katika dimba la ligi kuu ya NBC Tanzania:

Yanga SC vs Pamba Jiji – Saa 1:00 usiku (Benjamin Mkapa Stadium).

Hii ni mechi ya ufunguzi wa msimu wa 2025/2026 kwa mabingwa watetezi Yanga SC. Mashabiki wanatarajia kuona jeuri ya mabingwa hawa ikikabiliana na wapinzani wapya Pamba Jiji.

Azam FC vs Mbeya City – Saa 3:00 usiku (Azam Complex).

Azam FC, maarufu kama Wana Lambalamba, wataingia dimbani kwa mara ya kwanza msimu huu wakikabiliana na Mbeya City, timu inayojulikana kwa upinzani mkali kila inapokutana na wakubwa wa ligi.

Michezo hii yote ya ligi kuu ya NBC Tanzania itarushwa moja kwa moja kupitia Azam Sports 1HD.

Ratiba ya Mechi za Leo 24/09/2025

Ratiba ya UEFA Europa League (Ulaya)

Michuano ya Europa League inatarajiwa kua na upinzani mkali leo, huku timu maarufu barani Ulaya zikichuana vikali:

  • PAOK vs Maccabi Tel Aviv – Saa 19:45
  • Midtjylland vs Sturm Graz – Saa 19:45
  • Dinamo Zagreb vs Fenerbahçe – Saa 22:00
  • Real Betis vs Nottingham Forest – Saa 22:00
  • Malmö FF vs Ludogorets – Saa 22:00
  • Freiburg vs Basel – Saa 22:00
  • Braga vs Feyenoord – Saa 22:00
  • Nice vs AS Roma – Saa 22:00
  • Crvena Zvezda vs Celtic – Saa 22:00

Ratiba ya La Liga Hispania

Mashabiki wa ligi ya Uhispania (La Liga) pia hawatabaki nyuma, kwani mechi kadhaa imepangwa kupigwa leo usiku:

  • Getafe vs Alavés – Saa 20:00
  • Atlético FC vs Rayo Vallecano – Saa 22:30
  • Real Sociedad vs Mallorca – Saa 22:30

Ratiba ya CAF Champions League (Afrika)

Katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya Ivory Coast, Stade Abidjan, itakuwa mwenyeji wa Côte d’Or kutoka Shelisheli:

  • Stade Abidjan vs Côte d’Or – Saa 19:00

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Fadlu Davids Atambulishwa Kama Kocha Mkuu wa Raja Casablanca ya Morocco
  2. Lamine Yamal Abeba Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka (Kopa Trophy)
  3. Simba Yamtambulisha Hemed Suleiman Kama Kocha wa Mpito
  4. Ousmane Dembélé Ashinda Tuzo ya Ballon d’Or 2025
  5. Ratiba ya Mechi za Leo 22/09/2025
  6. Matokeo ya Gaborone United vs Simba leo 20/09/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo