Ratiba ya Mechi za Leo Ligi Kuu ya NBC 22/06/2025

Ratiba ya Mechi za Leo Ligi Kuu ya NBC 22/06/2025

Leo Juni 22, 2025 ni moja kati ya siku ambazo wapenzi wengi wa soka nchini wamekuwa wakingoja kwa hamu kubwa. Ni siku ya mwisho kwa michezo ya raundi ya 30 ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 michezo ambayo ina nafasi ya kubadili mwelekeo mzima wa ubingwa, nafasi za juu, nafasi za kushiriki mashindano ya kimataifa, pamoja na mapambano ya kusalia ligi kuu msimu ujao.

Kwa mujibu wa ratiba rasmi iliyotolewa na Bodi ya Ligi, jumla ya mechi nane zinachezwa leo kwa wakati mmoja, saa 10:00 jioni, kwenye viwanja mbalimbali nchini. Hii hapa ni ratiba ya mechi za leo Ligi Kuu ya NBC 22/06/2025:

Ratiba Kamili ya Ligi Kuu ya NBC Mechi za Leo (22 Juni 2025)

Mechi Saa Cheneli Inayoonesha
Mashujaa FC vs JKT Tanzania 10:00 Jioni Sinema Zetu
Pamba Jiji vs KMC FC 10:00 Jioni UTV
Simba SC vs Kagera Sugar 10:00 Jioni Azam Sports 2 HD
Namungo vs KenGold 10:00 Jioni TV TWO
Singida BS vs Tanzania Prisons 10:00 Jioni Azam Sports ONE
Young Africans vs Dodoma Jiji 10:00 Jioni Azam Sports 1
Coastal Union vs Tabora United 10:00 Jioni ZBC2
Fountain Gate vs Azam FC 10:00 Jioni Azam Sports 3

Ratiba ya Mechi za Leo Ligi Kuu ya NBC 22/06/2025

Umuhimu wa Michezo ya Leo: Vita za Ubingwa, Kushuka Daraja na Tuzo Binafsi

Vita ya Ubingwa Bado Imara

Mabingwa watetezi, Young Africans (Yanga) wakiwa na alama 76, wanahitaji ushindi ili kulinda nafasi yao ya kwanza mbele ya Simba SC, waliopo nafasi ya pili kwa pointi 75. Timu zote zimecheza mechi 28, hivyo leo ni mechi ya 29 kabla ya kukamilisha msimu kwa mechi ya kiporo baina yao Juni 25, 2025.

Mapambano ya Kubaki Ligi Kuu

Timu kama Tanzania Prisons, Namungo, na Fountain Gate ziko katika hali ya tahadhari kubwa. Fountain Gate tayari imeingia kwenye nafasi ya mtoano, lakini ushindi dhidi ya Azam unaweza kubadili hesabu. Prisons na Namungo zinahitaji matokeo mazuri ili kuepuka nafasi hizo hatari.

  • Tanzania Prisons (Pointi 30) inahitaji ushindi dhidi ya Singida BS na matumaini ya Pamba Jiji kupoteza ili iweze kuepuka mtoano.
  • Namungo (Pointi 32) itavaana na KenGold iliyoshuka daraja lakini bado ni tishio kutokana na uzoefu wa mechi zao zilizopita dhidi ya Kagera Sugar.

Nani Atatwaa Kiatu cha Dhahabu?

Straika wa Simba, Jean Charles Ahoua, anaongoza katika orodha ya wafungaji akiwa na mabao 16. Anawania tuzo ya mfungaji bora dhidi ya wapinzani wake kama Clement Mzize, Prince Dube (Yanga), na Leonel Ateba (Simba) wenye mabao 13 kila mmoja.

Tuzo ya Kipa Bora

Mchezaji mwingine aliye karibu kutwaa tuzo ni Moussa Camara (Simba SC), mwenye clean sheets 18. Djigui Diarra wa Yanga akiwa na clean sheets 16 bado ana nafasi ya kumfikia endapo atacheza kwa ubora leo na katika mechi ya kiporo.

Takwimu Muhimu Msimu wa 2024/2025

  1. Mabao yaliyofungwa hadi sasa ni 544, yakizidi 517 ya msimu uliopita.
  2. Hat trick nne tu zimepatikana msimu huu, chini ukilinganisha na saba za msimu uliopita.
  3. Penalti 87 zimeshapigwa msimu huu, karibu mara mbili ya 48 za msimu uliopita.
  4. Kadi nyekundu 21 tayari zimetolewa, sawa na msimu uliopita.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga VS Dodoma Jiji Leo 22/06/2025
  2. Matokeo ya Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025
  3. Kikosi cha Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025
  4. Simba Vs Kagera Sugar Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?
  5. Yanga vs Dodoma Jiji Leo 22/06/2025 Saa Ngapi?
  6. TFF Yafunga Rasmi Zoezi la Uchukuaji wa Fomu za Uongozi – Wagombea 25 Wajitokeza
  7. Tanzania Yashinda Ubingwa wa CECAFA Wanawake 2025 Kupitia Twiga Stars
  8. KMKM Mabingwa wa FA Cup Zanzibar 2025 Baada ya Ushindi wa 4-2 Dhidi ya Chipukizi
  9. Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
  10. Klabu ya Liverpool Yamwaga Mamilioni Kumnasa Florian Wirtz
  11. Viingilio Simba SC vs Kagera Sugar 22/06/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo