Ratiba ya Mtihani Darasa la Saba 2024
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) almaharufu kama mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2024. Mtihani huu ni hatua muhimu kwa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi, na utachukua siku mbili kufanyika kuanzia Jumatano, Septemba 11, 2024 hadi Alhamisi, Septemba 12, 2024.
Kwa wazazi, walimu, na wadau mbalimbali, ratiba hii ni nyenzo muhimu kwa maandalizi bora ya wanafunzi. Hapa chini tumetoa maelezo ya kina ya ratiba ya mtihani huu, pamoja na hatua za kujiandaa na mambo muhimu ya kuzingatia kwa wanafunzi.
Ratiba Kamili ya Mtihani wa Darasa la Saba 2024
Siku ya Kwanza: Jumatano, Septemba 11, 2024
- Saa 2:00 – 3:40 Asubuhi: Somo la Kiingereza
- Saa 3:40 – 4:30 Asubuhi: Mapumziko
- Saa 4:30 – 6:00 Mchana: Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi
- Saa 6:00 – 8:00 Mchana: Mapumziko (Chakula cha Mchana)
- Saa 8:00 – 9:30 Jioni: Sayansi na Teknolojia
Siku ya Pili: Alhamisi, Septemba 12, 2024
- Saa 2:00 – 4:00 Asubuhi: Hisabati
- Saa 4:00 – 5:00 Asubuhi: Mapumziko
- Saa 5:00 – 6:40 Mchana: Kiswahili
- Saa 6:40 – 8:30 Mchana: Mapumziko (Chakula cha Mchana)
- Saa 8:30 – 10:00 Jioni: Uraia na Maadili
Vidokezo Muhimu kwa Wanafunzi na Wazazi
Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Mtihani ya mwaka 2024 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
Hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kuthibitisha kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Mtihani.
Kabla ya kufungua bahasha, mpe Mtahiniwa asome kwa sauti jina la somo lililoandikwa juu ya bahasha ili kuthibitisha ni somo husika kwa mujibu wa ratiba.
Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo katika Karatasi ya Mtihani na Ratiba ya Mtihani, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya Mtihani husika ndiyo yatakayofuatwa.
Watahiniwa wenye mahitaji Maalum (Wasioona, Uoni hafifu, Viziwi) waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa somo la Hisabati na DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa masomo mengine.
Watahiniwa wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za Mtihani zenye maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.
Watahiniwa waelekezwe;
- Kuingia ndani ya chumba cha Mtihani nusu saa kabla ya muda wa Mtihani na watakaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya Mtihani kuanza hawataruhusiwa.
- Kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa Mtihani. Kuandika namba ya Mtihani kwa usahihi.
- Kutofanya mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina yao. Ikiwa Mtahiniwa ana tatizo anatakiwa kunyoosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa Mtihani.
- Kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani kwani watakaojihusisha matokeo yao yatafutwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti