Ratiba ya Taifa Stars vs DR Congo Kufuzu AFCON 2025 | Tanzania Taifa Stars Vs DR Congo Ni Lini na Saa Ngapi?
Ratiba ya Taifa Stars vs DR Congo Kufuzu AFCON 2025
Kuelekea mechi za kuwania tiketi ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), Timu ya Taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, inajiandaa kwa michezo miwili muhimu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo). Mechi hizi zitafanyika mnamo Oktoba 10 na Oktoba 15, 2024, ambapo Taifa Stars itaanza ugenini kabla ya kurudi nyumbani kwa mchezo wa marudiano.
Tanzania Taifa Stars Vs DR Congo Ni Lini na Saa Ngapi?
Mechi ya kwanza- DR Congo vs Tanzania
- Alhamisi, 10 Oktoba 2024
- Saa 1:00 Usiku (19:00) kwa saa za DR Congo
Mechi ya Pili- Tanzania vs DR Congo
- Jumanne, 15 Oktoba 2024
- Saa 10:00 Alasiri (16:00) kwa saa za Afrika Mashariki
Maandalizi ya Taifa Stars Kuelekea Michezo Miwili Dhidi ya DR Congo
Kocha wa muda wa Taifa Stars, Hemed Morocco, ametangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki katika maandalizi ya michezo hii miwili. Timu ya Tanzania ipo kundi H na ina pointi nne baada ya kutoka sare na Ethiopia na kuwashinda Guinea. Hii inaipa Taifa Stars nafasi nzuri ya kuendelea kupambana na kushinda michezo dhidi ya DR Congo ili kujihakikishia kufuzu kwa AFCON 2025.
Kwa upande wa DR Congo, wanashikilia nafasi ya kwanza katika kundi hilo wakiwa na pointi sita, jambo linaloashiria umuhimu wa mechi hizi kwa Taifa Stars. DR Congo ni timu yenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika, hivyo Kocha Morocco pamoja na timu yake ya ufundi wamefanya kazi kubwa kuhakikisha wanafanya uchaguzi wa wachezaji sahihi kwa ajili ya mechi hizi.
Kikosi na Mbinu za Kocha Hemed Morocco
Kocha Hemed Morocco amechagua mchanganyiko wa wachezaji wazoefu na vijana wenye damu ya moto. Nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Samatta, anarudi kwenye timu baada ya kukosa mechi dhidi ya Ethiopia na Guinea. Uzoefu wa wachezaji kama Samatta utaongeza nguvu na uongozi kwa vijana wanaochipukia kwenye timu kama vile Novatus Dismas, mchezaji anayechukuliwa kama kipaji kipya cha kuangaliwa.
Morocco amesema, “Tumezingatia uwezo wa kila mchezaji na jinsi wanavyoweza kuchangia kwenye mbinu zetu kwa ajili ya michezo hii. Ni muhimu tukafanikisha lengo letu la kufuzu, na tunaamini kikosi hiki kitafanya vizuri.”
Ujumuishaji wa wachezaji chipukizi ni mkakati wa Kocha Morocco kuhakikisha timu ina kasi na ubunifu, huku wachezaji wazoefu wakisaidia kuleta utulivu na mbinu za kukabiliana na timu yenye uzoefu kama DR Congo.
Angalia Hapa Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Dhidi ya DR Congo Kufuzu AFCON 2025
Umuhimu wa Ushindi kwa Taifa Stars
Ushindi katika mechi hizi mbili ni muhimu sana kwa Taifa Stars ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu moja kwa moja kwa michuano ya AFCON 2025. Taifa Stars inatakiwa kutumia vyema faida ya kucheza nyumbani kwenye mchezo wa marudiano ili kuhakikisha wanapata matokeo bora. Mashabiki wa Tanzania wana matumaini makubwa kwa timu yao, wakiamini kwamba kupitia maandalizi na ushirikiano kati ya wachezaji, Taifa Stars inaweza kufanya vizuri.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti