Serikali Yaahidi Sh1 Bilioni kwa Taifa Stars Wakitwaa Kombe la CHAN 2024

Serikali Yaahidi Sh1 Bilioni kwa Taifa Stars Wakitwaa Kombe la CHAN 2024

Katika kuongeza hamasa na kuleta ari mpya ya ushindi kwenye Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) mwaka 2024, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kitita cha Shilingi bilioni moja kwa wachezaji wa Timu ya Taifa, Taifa Stars, endapo watafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 2 hadi 30 Agosti 2024, huku Tanzania ikiwa mwenyeji pamoja na mataifa jirani ya Kenya na Uganda.

Serikali Yaahidi Sh1 Bilioni kwa Taifa Stars Wakitwaa Kombe la CHAN 2024

Ahadi ya Rais Samia kwa Taifa Stars CHAN 2024

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Palamagamba Kabudi, alitangaza rasmi ahadi hiyo ya fedha kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika hotuba yake, Kabudi alisema:

“Katika kuchagiza hamasa kwa timu yetu ya Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi ya donge nono la fedha za Kitanzania Sh1 bilioni kwa vijana wetu wa Taifa Stars iwapo watafanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano haya ya CHAN 2024.”

Ahadi hiyo inalenga kuongeza morali kwa wachezaji na benchi la ufundi katika maandalizi yao kuelekea michuano hiyo mikubwa ya kimataifa.

Tanzania Mwenyeji wa CHAN 2024 – Maandalizi Yapo Imara

Kwa mara ya kwanza, Tanzania itakuwa mwenyeji mwenza wa mashindano ya CHAN kwa kushirikiana na Kenya na Uganda. Waziri Kabudi alieleza kuwa maandalizi yamefikia hatua ya kuridhisha, ambapo jumla ya hatua nane muhimu zimeshakamilika kwa upande wa Tanzania.

Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na:

  1. Kukamilika kwa malipo ya ada ya ushiriki na maandalizi.
  2. Ukarabati na uboreshaji wa viwanja vya mashindano na mazoezi kwa asilimia 100 jijini Dar es Salaam na Zanzibar.
  3. Kuundwa kwa kamati za kitaifa za maandalizi.
  4. Kuimarishwa kwa maandalizi ya kikosi cha Taifa Stars.
  5. Kujengewa uwezo kwa wataalamu wa uratibu na usimamizi.
  6. Kutengenezwa kwa mkakati wa hamasa na utangazaji wa mashindano.
  7. Kuandaliwa huduma za kijamii kama malazi, usafiri, na huduma za afya kwa wageni, timu na viongozi wa CAF.
  8. Kukamilishwa kwa maandalizi kuelekea mechi ya ufunguzi.

Ratiba ya Taifa Stars CHAN 2024 na Kundi B

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepangwa Kundi B pamoja na mataifa ya Burkina Faso, Madagascar, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mauritania. Mechi zao zote zitachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa ufunguzi wa Taifa Stars unatarajiwa kuchezwa tarehe 2 Agosti 2024 dhidi ya Burkina Faso. Viingilio vya mashabiki kwa mechi hizo vitaanza kutoka Sh2,000 kwa jukwaa la mzunguko, Sh5,000 kwa VIP B na Sh10,000 kwa VIP A.

Wito kwa Watanzania: Changamkieni Fursa na Kuipa Taifa Stars Sapoti

Mbali na hamasa ya Sh1 bilioni kwa Taifa Stars, Waziri Kabudi pia alitoa wito kwa Watanzania wote kutumia kikamilifu fursa za kiuchumi na kibiashara zitakazopatikana kupitia mashindano haya ya kimataifa. Aliwahimiza wananchi kushiriki katika sekta kama vile utalii, usafirishaji, malazi, huduma za chakula na burudani ili kujipatia kipato kupitia wageni wanaotarajiwa kuja kushuhudia mashindano hayo.

Amesema: “Nitumie fursa hii kutoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara na kiuchumi zinazoambatana na mashindano haya, ikiwemo malazi, utalii, vyakula na usafirishaji.”

Aidha, aliwataka mashabiki wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi viwanjani kuisapoti Taifa Stars, huku akiunga mkono kaulimbiu rasmi ya mashindano kwa upande wa Tanzania: “LINAKUJA NYUMBANI.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
  2. Wachezaji Wapya wa Yanga 2025/2026
  3. Cv ya Romain Folz Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026
  4. Tetesi za Usajili Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026
  5. Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
  6. CV ya Moussa Balla Conte Mchezaji Mpya wa Yanga Sc 2025/2026
  7. Rasmi: Namungo FC Yathibitisha Kuachana na Mshambuliaji Meddie Kagere
  8. Kikosi cha Taifa Stars Kinaendelea Kujifua Nchini Misri kwa Ajili ya CHAN 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo