Shauri la Yanga CAS Lapigwa Chini, Kariakoo Derby kupangiwa Tarehe

Shauri la Yanga CAS Lapigwa Chini

Shauri la Yanga CAS Lapigwa Chini, Kariakoo Derby kupangiwa Tarehe

Shauri lililowasilishwa na klabu ya Young Africans (Yanga) katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) likiwa na lengo la kuzuia upangaji wa tarehe mpya ya mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC, pamoja na kudai pointi za mezani, limefutwa rasmi. Uamuzi huo umetolewa baada ya CAS kubaini kuwa Yanga haikufuata taratibu za ndani za malalamiko kabla ya kukimbilia mahakama hiyo ya kimataifa.

Awali, mchezo huo maarufu wa Kariakoo Derby uliokuwa umepangwa kuchezwa Machi 8, 2025, uliahirishwa kufuatia Simba SC kuzuiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, siku moja kabla ya pambano. Kutokana na tukio hilo, Yanga iliwasilisha rufaa CAS ikitaka kupewa ushindi wa mezani na kucheleweshwa kwa upangaji wa tarehe mpya ya mchezo.

Shauri la Yanga CAS Lapigwa Chini, Kariakoo Derby kupangiwa Tarehe

Hata hivyo, CAS imeamua kutupilia mbali rufaa hiyo kwa misingi ya kisheria, ikibainisha kuwa Yanga ilipaswa kwanza kufuata mchakato wa malalamiko ndani ya vyombo vya soka vya ndani. Kulingana na maelezo ya CAS, rufaa hiyo haikupaswa kupokelewa kwa kuwa haikupitia Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kama inavyotakiwa na Ibara ya 37 ya kanuni husika.

“Naibu Rais anaona kuwa njia sahihi ya kukata rufaa ya Mrufani iko mbele ya Kamati ya Rufani ya TFF, na kwamba Mrufani alishindwa kutumia masuluhisho yote ya ndani ya kisheria,” imesema taarifa ya CAS.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, Mahakama hiyo imehitimisha kuwa haina mamlaka ya kisheria kushughulikia shauri hilo la Yanga dhidi ya TFF, Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), na Simba SC. Hii ina maana kuwa kesi namba CAS 2025/A/11298 imeondolewa rasmi na kuondolewa katika orodha ya mashauri ya CAS kwa mwaka huo.

Katika hatua ya haraka kufuatia uamuzi wa CAS, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kupitia taarifa yake imetangaza kuwa inaendelea na maandalizi ya kupanga tarehe mpya ya mchezo huo wa Derby ya Kariakoo.

“Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inaendelea na maandalizi yake ya kuhitimisha msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 na kufanya maboresho ya ratiba ya Ligi (ukiwemo mchezo namba 184 – Young Africans vs Simba SC) kisha kutangaza ratiba mpya mapema iwezekanavyo,” imesema TPLB.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kipagwile Aibuka Mchezaji Bora Ligi Kuu April 2025, Ambwaga Pacome
  2. Guardiola Atangaza Kupumzika Ukocha Baada ya Mkataba Wa Man City Kuisha
  3. Ratiba ya Kombe la Muungano 2025
  4. Simba SC Yatinga Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Baada ya Sare na Stellenbosch
  5. Mayele Aipeleka Pyramid Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF
  6. Al Ahly Yamtimua Kocha Marcel Koller Baada ya Kutolewa Klabu Bingwa Afrika
  7. Mtibwa Sugar Yarejea Ligi Kuu NBC 2025/2026
  8. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2025
  9. JKU Yaiondoa Singida Black Stars Kombe la Muungano
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo