Sifa za Kujiunga na Jeshi la Magereza Tanzania 2025
Jeshi la Magereza ni miongoni mwa vyombo muhimu vya ulinzi na usalama nchini Tanzania, lenye jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa jamii kupitia usimamizi wa wafungwa na watuhumiwa walioko chini ya ulinzi wa kisheria.
Liliundwa rasmi tarehe 25 Agosti 1931, baada ya kutenganishwa kwa majukumu kati ya Jeshi la Polisi na Idara ya Magereza. Kabla ya mwaka huo, Jeshi la Polisi ndilo lililokuwa likisimamia pia kazi za magereza kwa mujibu wa mfumo wa kikoloni.
Mara baada ya kuanzishwa, Jeshi hili lilijulikana kama Idara ya Jela, ambapo awali shughuli zake zilijikita zaidi katika taratibu za kikoloni, ikiwemo utesaji na kazi ngumu kwa wafungwa bila kuzingatia manufaa ya taifa au ya wahusika.
Hata hivyo, mabadiliko makubwa yamefanyika kadri miaka ilivyosonga, na leo hii Jeshi la Magereza limejikita katika urekebishaji wa tabia, kutoa elimu na stadi za maisha kwa wafungwa, pamoja na kulinda usalama wa raia.
Majukumu Makuu ya Jeshi la Magereza
Jeshi la Magereza Tanzania lina majukumu kadhaa muhimu kwa ustawi wa taifa, ikiwemo:
- Kuwahifadhi wafungwa wa aina zote waliowekwa chini ya ulinzi halali wa kisheria.
- Kuandaa na kutekeleza programu za urekebishaji, ikiwa ni pamoja na kuwafundisha wafungwa ujuzi mbalimbali wa uzalishaji na maisha.
- Kutoa huduma kwa mahabusu kwa kuzingatia misingi ya kisheria na haki za binadamu.
- Kuchangia katika ushauri wa kitaifa kuhusu njia bora za kuzuia na kudhibiti uhalifu.
Kwa njia hii, Jeshi la Magereza husaidia kulinda jamii na kuhakikisha kuwa wafungwa wanapata nafasi ya kubadilika na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi mara baada ya kuachiwa huru.
Sifa za Kujiunga na Jeshi la Magereza Tanzania 2025
Kwa vijana wanaotamani kujiunga na Jeshi la Magereza mwaka 2025, kuna masharti na vigezo rasmi vinavyopaswa kuzingatiwa.
Zifuatazo hapa chini ni sifa kuu zinazohitajika:
1. Lazima uwe Raia wa Tanzania.
2. Unatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Uraia au Namba ya NIDA.
3. Usiwahi kuajiriwa katika taasisi yoyote ya Serikali.
4. Umri:
- Wahitimu wa Kidato cha Nne wanatakiwa kuwa na umri kati ya miaka 18 na 24.
- Wenye ujuzi maalum wanatakiwa kuwa na umri kati ya miaka 18 na 28.
5. Lazima uwe na cheti halisi cha kuzaliwa.
6. Urefu:
- Wanaume wanatakiwa kuwa na urefu usiopungua futi 5’7”.
- Wanawake wanatakiwa kuwa na urefu usiopungua futi 5’4”.
7. Uwe na siha njema ya mwili na akili, iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
8. Hutakiwi kuwa umeoa au kuolewa, na wanawake hawatakiwi kuwa wamejifungua.
9. Ili kujiunga na jeshi la magereza hutakiwi kua na alama au michoro yoyote (tattoo) mwilini.
10. Lazima uwe na nidhamu na tabia njema, na usiwe umewahi kupatikana na hatia ya jinai au kufungwa gerezani.
11. Ni lazima uwe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Askari Magereza na kufanya kazi popote Tanzania Bara.
12. Unatakiwa kuwa tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili hadi utakapofika mafunzoni.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Nafasi Mpya za Kazi MDAs & LGAs Juni 2025 – Tangazo la Ajira Serikalini Nafasi 6,732
- Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la JWTZ
- Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
- Rais Samia Atangaza Ongezeko Kubwa la Mishahara kwa Watumishi wa Umma
- Kiwango Cha Chini Cha Mshahara Kwa Watumishi wa Umma Chapanda Hadi 500,000
- Ratiba ya Usaili Wa Mahojiano TRA 2025
- Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania April 2025
Leave a Reply