Siku ya Kuripoti Shule Kidato cha Kwanza 2026
Wanafunzi 937,581, sawa na asilimia 100 ya wote waliohitimu kwa sifa stahiki, wameteuliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2026 baada ya kupangiwa shule za serikali katika mikoa na halmashauri mbalimbali nchini. Kundi hili linajumuisha wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2025 na kupata alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300.
Akitoa taarifa hii jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe, amesema serikali imehakikisha kila mwanafunzi mwenye sifa amepangiwa shule kulingana na mfumo wa ugawaji nafasi kitaifa.
“Kila mwanafunzi aliyefanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2025 na kupata alama kati ya 121 na 300 amechaguliwa na kupangiwa shule ya serikali,” amesema Prof. Shemdoe.
Taarifa hii imekuja katika kipindi ambacho wazazi na walezi wanajiandaa kuhakikisha wanafunzi wanaripoti shuleni kwa wakati na kuendelea na masomo hadi kumaliza Kidato cha Nne.
Siku ya Kuripoti Shule Kidato cha Kwanza 2026
Kwa mujibu wa maelezo ya Prof. Shemdoe:
- Shule za bweni: Wanafunzi wote waliopangiwa bweni wanatakiwa kuripoti tarehe 12 Januari 2026.
- Shule za kutwa: Wanafunzi waliopangiwa mfumo wa kutwa wanatakiwa kuripoti tarehe 13 Januari 2026.
Tarehe hizi ni muhimu kwa wanafunzi wote waliochaguliwa, hivyo wazazi wanashauriwa kuhakikisha maandalizi yanakamilika mapema.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply