Simba Imetangaza Kuachana na Shaban Chilunda
Dar es Salaam, Tanzania – Klabu ya soka ya Simba imetangaza rasmi kuachana na mshambuliaji wake mahiri, Shaban Idd Chilunda. Hatua hii inakuja baada ya kumalizika kwa mkataba wa mwaka mmoja wa Chilunda na Wekundu wa Msimbazi, na hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi chao katika msimu wa ligi 2024/25.
Chilunda alijiunga na Simba mwaka 2023 akitokea Azam FC, akitazamiwa kuwa tegemezi kubwa kwa klabu kupitia kipaji chake na kuchangia mafanikio ya klabu. Licha ya kuanza kwa kasi, mchango wake ulionekana kupungua kadri msimu ulivyosonga mbele.
Simba Imetangaza Kuachana na Shaban Chilunda
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti