Simba Kususia Dabi Nyingine Kama Yanga Hawatoshiriki Mchezo wa June 15
Kuelekea mvutano unaoendelea baina ya Yanga SC, TFF na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuhusu msimamo wa Yanga wa kutoshiriki mchezo wa Dabi ya Kariakoo uliopangwa kufanyika Juni 15, 2025, Klabu ya Simba SC imeibuka na msimamo mzito.
Simba kupitia taarifa rasmi iliyotolewa tarehe 12 Juni 2025, imetangaza kuwa itapeleka timu yake uwanjani siku ya Jumapili, Juni 15 kushiriki katika mchezo huo wa namba 184 kama ulivyopangwa awali. Hata hivyo, Simba imesisitiza kuwa haitashiriki mchezo huo iwapo utabadilishwa tarehe au kuahirishwa tena.
Katika taarifa hiyo iliyochapishwa kupitia mitandao rasmi ya klabu, Simba SC imesema wazi kuwa jaribio lolote la kuahirisha mchezo huo ni batili na kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu nchini Tanzania.
“Klabu ya Simba inauarifu umma, wanachama na wapenzi wake kuwa itaingia uwanjani siku ya Jumapili, tarehe 15 Juni 2025, kushiriki mchezo namba 184 kama ilivyopangwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.”
Simba Yashikilia Msimamo Mkali – Hakuna Mabadiliko ya Ratiba
Taarifa hiyo imeweka wazi kuwa mabadiliko yoyote ya tarehe ya mchezo huo hayatakubalika. Simba imeeleza kuwa haitashiriki mchezo wa namba 184 endapo hautachezwa siku ya Jumapili, Juni 15 kama ilivyopangwa.
“Mabadiliko yoyote ya kujaribu kuahirisha mchezo huo ni batili na kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu. Kwa msingi huo, Klabu ya Simba haitashiriki mchezo wowote wa namba 184 isipokuwa ule uliopangwa kuchezwa siku ya Jumapili, tarehe 15 Juni 2025.”
Kauli hii inakuja siku chache kabla ya tarehe ya mchezo huku kukiwa na sintofahamu kuhusu ushiriki wa Yanga SC, ambao awali walitangaza kutoshiriki kutokana na malalamiko yao dhidi ya baadhi ya maamuzi ya Bodi ya Ligi na TFF.
Mashabiki Watahimizwa Kujitokeza Kwa Wingi Benjamin Mkapa
Mbali na msimamo huo, Simba SC imewataka wanachama na mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kuujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa katika siku hiyo muhimu ili kuisapoti timu yao, ikisisitiza kuwa uwepo wao ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki cha mvutano mkubwa kwenye soka la Tanzania.
“Tunawaomba wanachama na wapenzi wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kuijaza Benjamin Mkapa siku hiyo muhimu ili kuiunga mkono timu yetu.”
Mapendekezo ya Mhariri:
- Timu Zilizofuzu Nusu Fainali COSAFA Cup 2025
- Taifa Stars Yaaga COSAFA Cup Licha ya Kuifunga Eswatini 2-1
- Tijjani Reijnders Asaini Manchester City Miaka Mitano Akitokea AC Milan
- Serikali Yajieka Pembeni na Sakata la dabi, yawaachia TFF
- Chelsea Yathibitisha Kumsajili Beki Mamadou Sarr Kutoka Strasbourg
- Yanga Kususia Fainali CRDB FA Cup Kisa Madeni ya Msimu Uliopita
- Yanga Yaibua Mambo Mapya Wakizungumzia Sakata la Dabi
Leave a Reply