Simba vs Mbeya City Leo 04/12/2025 Saa Ngapi?

Simba vs Mbeya City Leo 04/12/2025 Saa Ngapi?

Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo watakuwa dimbani kuwakabili Mbeya City FC katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu ya NBC, pambano ambalo limepangwa kufanyika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam. Mtanange huu wa Alhamisi unatarajiwa kuwa miongoni mwa michezo yenye ushindani mkubwa, ukizingatia matamko kutoka kwa benchi la ufundi la timu zote mbili.

Mchezo Simba vs Mbeya City leo 04/12/2025 utapigwa Saa 1:00 usiku, na utarushwa mubashara kupitia AzamSports1HD.

Saa Ngapi Simba vs Mbeya City Leo?

  • Tarehe: 04/12/2025
  • Muda: Saa 1:00 usiku
  • Mahali: Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam
  • Channel: AzamSports1HD

Simba vs Mbeya City Leo 04/12/2025 Saa Ngapi?

Huu ni mchezo wa mwendelezo wa Ligi Kuu NBC ambapo Simba wanawakaribisha The Purple Nation – Mbeya City, wakilenga kuendeleza kasi ya kutafuta pointi muhimu kwenye mbio za ubingwa.

Maandalizi ya Simba SC Kabla ya Mchezo

Kocha wa Simba, Selemani Matola, ameeleza kuwa timu imefanya maandalizi ya kina kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu. Amedokeza kuwa hakuna mechi rahisi katika ligi, na hivyo wanatarajia mchezo wenye changamoto.

“Kwenye ligi hakuna timu nyepesi. Mbali ya ugumu huo tumejipanga na kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kushinda na kupata pointi tatu kwenye mchezo wa kesho,” amesema Matola.

Kauli hii inaonyesha dhamira ya Simba kuingia na nguvu mpya, hasa wakijua kuwa wapinzani wao wamedhamiria kujibu mapigo licha ya changamoto walizokutana nazo msimu huu.

Mbeya City Wakitazama Mchezo Kama Fursa ya Kufufua Matumaini

Kaimu Kocha Mkuu wa Mbeya City, Patrick Mwangata, amesema kikosi chake hakitakubali kuendelea na mwenendo wa kupoteza mechi mfululizo. Licha ya kutokea katika mazingira magumu, wamesisitiza kuwa wanajipanga kuondoka na furaha.

“Tunajua kwetu ni mchezo mgumu sana kwa sababu tumetoka kupoteza mechi tatu mfululizo. Tunawaheshimu lakini sisi kama Mbeya City tumejiandaa vizuri kuhakikisha mchezo wa kesho, tunafanya vizuri,” amesema Mwangata.

Kauli hiyo inaweka bayana kuwa Mbeya City wanaingia katika mchezo huu wakiwa na presha ya kutafuta matokeo, jambo linaloweza kuongeza ushindani ndani ya dakika 90.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo Wa Championship Ligi Daraja la Kwanza Tanzania 2025/2026
  2. Msimamo wa Kundi la Azam Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
  3. Simba Yachezea Kichapo cha Pili Mfululizo Makundi Klabu Bingwa
  4. Singida BS Yapata Pointi ya Kwanza Makundi Kombe la Shirikisho CAF
  5. Matokeo ya Stade Malien vs Simba leo 30/11/2025
  6. Kikosi cha Simba vs Stade Malien leo 30/11/2025
  7. Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Leo 30/11/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo