Simba Vs Singida Black Stars Leo 31/05/2025 Saa Ngapi?
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo tarehe 31 Mei 2025 wanashuka dimbani kuisaka nafasi ya kufuzu fainali nyingine ya Kombe la Shirikisho la CRDB, baada ya kutofanikiwa kutamba katika fainali za CAF msimu huu. Simba SC watakutana na Singida Black Stars katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, kuanzia saa 9:30 alasiri. Hii ni mechi ya tatu kwa msimu wa 2024/25 kwa timu hizi kukutana, baada ya michezo miwili ya ligi ambapo Simba SC walishinda mechi zote kwa bao 1-0. Mchezo huu wa nusu fainali unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa hasa kwa kuwa mshindi atakutana na Yanga SC kwenye fainali.
Kwa upande wa Simba SC, kiungo mshambuliaji Jean Ahoua ameonekana kuwa mwiba kwa Singida Black Stars. Katika michezo miwili ya ligi msimu huu, Ahoua ndiye aliyetoa pasi za mwisho zilizozaa mabao ya ushindi. Taarifa zinaonesha Ahoua ametengeneza pasi 8 za mabao na kufunga mabao 15 ndani ya msimu huu wa 2024/25.
Kwa upande wa Singida Black Stars, mshambuliaji Jonathan Sowah ndiye tegemeo kubwa katika safu ya ushambuliaji. Sowah ameifungia timu yake mabao 11 tangu alipojiunga katika dirisha dogo la usajili. Aidha, kiungo Kelvin Nashon atakuwa na kazi ya kukabiliana na viungo wa Simba SC, ingawa mara nyingi hujikuta akikumbana na adhabu ya kadi ya njano kutokana na aina yake ya ukabaji wa nguvu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Coastal Union Yapiga Hesabu Kali Kumchukua Anicet Kiazayidi
- Chelsea Yaipiga Bao Manchester United Usajili wa Liam Rory Delap
- Xabi Alonso Aahidi Kurejesha Ufalme wa Real Madrid
- Singida BS Yashindwa Kutamba Mbele ya Simba Ligi Kuu NBC
- Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 – Pakua PDF Hapa!
- Erik Ten Hag Atambulisha Rasmi Kama Kocha Mkuu Bayer Leverkusen
Leave a Reply