Simba vs TMA Stars Leo 11/03/2025 Saa Ngapi?

Simba vs TMA Stars Leo 11 03 2025 Saa Ngapi

Simba vs TMA Stars Leo 11/03/2025 Saa Ngapi?

Baada ya kushindwa kuchezwa kwa mechi ya Dabi ya Kariakoo wikiendi iliyopita dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu Tanzania Bara, leo jioni Simba SC inatarajiwa kushuka dimbani kukabiliana na TMA Stars ya Arusha katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho (FA). Mchezo huu utafanyika kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 jioni.

Muhtasari wa Mchezo Simba vs TMA Stars Leo

Simba vs TMA Stars Leo 11/03/2025 Saa Ngapi?

Simba SC, ambayo inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, itaingia uwanjani ikiwa na lengo la kusonga mbele katika michuano hii na kuweka rekodi nzuri kuelekea hatua za mwisho. TMA Stars, inayoshiriki Ligi ya Championship, ipo nafasi ya tano na ina matumaini ya kupambana vikali dhidi ya mabingwa hao wa zamani wa FA Cup.

Mchezo huu ni mojawapo ya mechi tatu za FA Cup zinazopigwa leo, huku Kiluvya United ikimenyana na Pamba Jiji, na Kagera Sugar ikiwa mwenyeji wa Namungo FC. Washindi wa mechi hizi watasonga mbele kwenye hatua ya 16 bora inayotarajiwa kuanza Alhamisi.

Je, Simba Itaendeleza Ubabe Wake?

Kwa upande wa Simba SC, wachezaji wake wa safu ya ushambuliaji wanatarajiwa kuwa na mchango mkubwa. Nyota kama Leonel Ateba, Jean Ahoua, na Steven Mukwala wamesajiliwa kwa ajili ya kufanikisha kampeni ya Simba msimu huu, na leo wanatarajiwa kuonyesha makali yao.

Simba imeonyesha ubora wake msimu huu kwa kufunga mabao 46 katika Ligi Kuu na kuruhusu mabao manane pekee, ikidhihirisha uimara wa safu yake ya ulinzi na ushambuliaji. Katika hatua ya 64 bora ya FA Cup, Simba iliichapa Kilimanjaro Wonders kwa mabao 6-1, hivyo itakuwa na ari kubwa kuendeleza mwendelezo huo wa ushindi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga VS Simba Leo 08/03/2025 Saa Ngapi?
  2. Mechi ya Leo ya Yanga Dhidi ya Simba Yaahirishwa
  3. Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 08/03/2025
  4. Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 08/03/2025
  5. Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya Yanga 08/03/2025
  6. Simba Yatangaza Kususia Mechi Dhidi ya Yanga Leo 08/03/2025: Nini Chanzo?
  7. Vituo Vya Kununua Tiketi za Mechi ya Yanga vs Simba 08/03/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo