Simba yamtambulisha Wilson Nangu

Simba yamtambulisha Wilson Nangu

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo wametangaza rasmi usajili wa beki wa kati wa Kitanzania, Wilson Edwin Nangu (23), akitokea JKT Tanzania. Usajili huu unakuja kama sehemu ya maandalizi ya klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hatua inayoongeza nguvu na ushindani kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria.

Nangu hakuchelewa kujipatia jina kubwa ndani ya JKT Tanzania, licha ya kujiunga nao kwa msimu mmoja pekee akitokea TMA ya Arusha. Mashabiki wa soka nchini bado wanakumbuka mchango wake kwenye mchezo dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC, uliomalizika kwa sare tasa (0–0). Katika mchezo huo, Nangu alionekana kuwa mwiba kwa washambuliaji wa Yanga na hata kuibuka nyota bora wa mchezo, jambo lililothibitisha uwezo wake mkubwa katika safu ya ulinzi.

Simba yamtambulisha Wilson Nangu

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu ya NBC 2025/2026
  2. Bayer Leverkusen Yamtimua Ten Hag Baada ya Mechi Tatu Tu
  3. Hizi Apa Picha za Jezi mpya za Simba 2025/2026
  4. Tarehe za Mechi za Simba VS Yanga 2025/2026: Ratiba ya Dabi ya Kariakoo
  5. Yanga Kutumia Benjamin Mkapa Kama Dimba la Nyumbani Huku Simba Kuhamia KMC Complex
  6. Msimamo wa Ligi Kuu England EPL 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo