Simba Yavizia Saini ya Issa Fofana Nchini Ivory Coast Kama Mrithi wa Camara
MABOSI wa Simba SC wameanza harakati kabambe za kuliboresha upya jeshi lao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC na michuano ya kimataifa, huku suala la mlinda mlango likibaki kuwa kitendawili kinachozua sintofahamu ndani ya kambi hiyo.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuachana na kipa wao namba moja, Moussa Camara, licha ya kuwa kinara wa clean sheets (19) msimu huu jambo ambalo limewafanya kugeuza macho yao hadi Ivory Coast kutafuta mbadala sahihi.
Katika kile kinachoonekana kama maandalizi ya mapema kwa ajili ya msimu mpya, Simba SC imeanza kumvizia kwa karibu kipa mahiri raia wa Ivory Coast, Issa Fofana, anayeichezea Al-Hilal Omdurman ya Sudan. Mabosi wa Wekundu wa Msimbazi wameripotiwa kuwa katika hatua za awali za kumsaka mchezaji huyo kama mrithi wa Camara, endapo nyota huyo kutoka Guinea ataondoka.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika, Fofana ameibuka kuwa chaguo la kwanza kutokana na uwezo wake mkubwa na umahiri wa kucheza soka la kisasa. Chanzo cha karibu na Simba kimeeleza kuwa:
“Ni kipa mdogo mwenye kipaji na kiwango bora sana. Tayari ameonyesha uwezo mkubwa akiwa na Al-Hilal, na tunahisi anaweza kuwa suluhisho la muda mrefu kwa Simba iwapo Camara ataondoka.”
Fofana alijiunga na Al-Hilal Omdurman mnamo Agosti 13, 2022, akitokea San Pedro ya kwao Ivory Coast, na mkataba wake unatarajiwa kuhitimishwa mnamo Juni 30, 2025. Hali hiyo imewafanya viongozi wa Simba kuanza kumuweka kwenye rada mapema ili wasibaki bila mbadala wa maana. Katika msimu huu wa ligi, Al-Hilal chini ya kocha Florent Ibenge ilishiriki Ligue 1 ya Mauritania, na kufanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kucheza mechi 30, kushinda 20, kutoka sare 7 na kupoteza michezo mitatu, ikiwa na jumla ya pointi 67.
Mafanikio hayo hayajapita kimya kwa Simba, ambao wamevutiwa na mchango wa Fofana katika mafanikio hayo ya timu.
Wakati juhudi hizo za kumvutia Fofana zikiendelea, ndani ya Simba bado kuna mjadala kuhusu kurejeshwa kwa kipa Ayoub Lakred ambaye kwa sasa amepona majeraha yaliyomweka nje kwa muda mrefu.
Lakred alijiunga na Simba mnamo Agosti 11, 2023, akitokea FAR Rabat ya Morocco, na mkataba wake unamalizika Juni 2025. Hata hivyo, nafasi yake kikosini bado ni finyu kutokana na ushindani na majeraha ya mara kwa mara.
Kile kinachoongeza ugumu ni taarifa kuwa klabu kadhaa kutoka Morocco zimeanza kumwinda tena Lakred, hali inayowafanya mabosi wa Simba kuwa na wakati mgumu wa kupanga mustakabali wa nafasi ya mlinda mlango namba moja.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
- Wydad Casablanca Yafungashiwa Virago Kombe la Dunia Bila Pointi
- Asante Kotoko Yachukua Nafasi ya Yanga Kombe la Toyota Afrika Kusini
- Milos Kerkez Ajiunga Rasmi na Liverpool kwa Ada ya Pauni Milioni 40
- Christian Eriksen Aondoka Man United Baada ya Utumishi wa Miaka Mitatu
- Kikosi cha Tanzania CHAN 2024: Wachezaji Kuingia Kambini Julai 7, 2025
- Yanga Yailaza Simba 2-0 na Kutwaa Kombe la Ligi Kuu Kwa Mara ya 31
- Vituo Vya Tiketi Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025
Leave a Reply