Stephane Aziz Ki Asaini Mkataba Mpya na Yanga SC
Wakatia mashabiki wa Yanga wakiendelea kufurahia utambulisho wa aliekua nyota wa Simba Sc Clatous Chama kama mchezaji mpya wa Yanga Sc kuelekea msimu wa 2024/2025, Leo julai 10 2024 klabu ya Yanga Sc imetangaza kufanikiwa kumshawishi kiungo mshambuliaji wao nyota, Stephane Aziz Ki kuongeza mkataba wake na klabu.
Aziz Ki amesaini mkataba mpya na klabu licha ya kuwepo kwa vilabu vikubwa barani Afrika ambavyo vilikua vinataka kumsajili master key. Baadhi ya vilabu ambavyo vilikua katika mchakato wa kumsaini Aziz ki ni pamoja na Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns, na Orlando Pirates.Β Taarifa ya Aziz ki kuendelea kubaki jangwani imeleta furaha kubwa kwa mashabiki wa klabu ya Yanga ambao wengi wao walionesha wazi kutaka kumuona nyota huyo akiitumikia klabu ya Yanga katika msimu mwingine zaidi.
Stephane Aziz Ki Asaini Mkataba Mpya na Yanga SC
ππππ ππππππ ππ @Aziz10Ki bado yupo sana Jangwani Wananchiπ°π
Taarifa zaidi tembelea Yanga SC APPπ²#TimuYaWananchi #DaimaMbeleNyumaMwiko pic.twitter.com/QDsxxayps2
β Young Africans SC (@YoungAfricansSC) July 10, 2024
Aziz Ki aliwasili Tanzania alfajiri ya Julai 10, 2024, akitokea mapumziko nchini kwao Burkina Faso kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia. Aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa usiri mkubwa.
Kwa kutumia mbinu maalum, alimtanguliza mfanyakazi mmoja wa uwanja wa ndege na mabegi yake sita makubwa. Ofisa wa Yanga, Godlisten Anderson βChicharitoβ, alikuja kumpokea na kumpa kofia maarufu ya kepu ili kujificha. Alipanda gari aina ya Toyota Alphard kisha kubadilisha magari akiwa njiani, na hatimaye akaondoka na gari aina ya Toyota Harrier.
Mafanikio ya Aziz Ki Yanga SC
Aziz Ki alikuwa mchezaji muhimu kwa Yanga msimu uliopita. Aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania akimaliza na mabao 21 na pasi za mwisho nane, hivyo kuiwezesha Yanga kutwaa ubingwa. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, alihusika na mabao manne, akifunga mawili na kupiga pasi mbili za mwisho, na kuisaidia Yanga kufikia hatua ya robo fainali.
Kiwango chake bora kimevutia klabu nyingi ndani na nje ya Afrika, ikiwa ni pamoja na Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns, na Orlando Pirates za Afrika Kusini, ambazo zote ziliwasilisha ofa za kumtaka.
Sababu za Yanga Kumbakisha Aziz Ki
- Kiwango Bora: Msimu uliopita, Aziz Ki alionesha kiwango cha juu kwa kufunga mabao muhimu na kutoa pasi za mwisho. Hii imemfanya kuwa mchezaji muhimu kwa Yanga.
- Ushawishi kwa Mashabiki: Aziz Ki amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga kutokana na mchango wake mkubwa katika mechi muhimu. Amefunga katika mechi nyingi dhidi ya wapinzani wa jadi, Simba SC na Azam FC.
- Historia ya Mafanikio: Tangu alipojiunga na Yanga mwaka 2022, Aziz Ki amekuwa na mchango mkubwa katika kuiwezesha timu kufikia mafanikio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
- Ushawishi kwa Vigogo wa Timu: Viongozi na wanachama wa Yanga wamekuwa na hamu kubwa ya kumbakisha Aziz Ki kutokana na ushawishi wake mkubwa ndani na nje ya uwanja.
Azma ya Yanga kwa Aziz Ki
Rais wa Yanga, Hersi Said, alibainisha kuwa klabu imeweka mkakati wa kuhakikisha Aziz Ki anabakia. Licha ya ofa nyingi kutoka klabu nyingine, Aziz Ki alionyesha nia ya kubaki Yanga na kuisaidia kufikia malengo yake. Hata hivyo, suala la kifedha linaweza kuathiri maamuzi ya mwisho. Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, alisisitiza umuhimu wa kumkuta Aziz Ki kambini mara atakapojiunga nayo, akionyesha kuwa bado anahitajika kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti