Dodoma Jiji FC Katika Mazungumzo ya Kumrejesha Wazir Jr
Wakati dirisha la usajili Ligi Kuu ya NBC Tnzania linapoelekea kufungwa, tetesi za sajili motomoto zinaendelea kushika kasi na hivi karibuni kumekua na uvumi wa kuwa Dodoma Jiji FC wapo kwenye mazungumzo ya kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani, Wazir Junior Shentembo. Wazir, ambaye alifunga mabao 12 msimu uliopita akiwa na KMC FC, amekuwa gumzo miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.
Dodoma Jiji, ambao walikuwa na msimu usiokua na mataokeo mazuri, wamepania kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao. Kurejea kwa Wazir Jr. kunaweza kuwa suluhisho la moja kwa moja kwa uhaba wa mabao walioupata msimu uliopita. Uwezo wake wa kufunga mabao na uzoefu katika Ligi Kuu ya NBC ni vitu ambavyo Dodoma Jiji wanavihitaji sana.
Wazir Jr. amethibitisha kuwa mmoja wa washambuliaji bora nchini. Msimu uliopita, alikuwa miongoni mwa wafungaji bora watatu katika Ligi Kuu, licha ya kucheza katika timu ambayo haikufanya vizuri sana. Uwezo wake wa kufunga mabao ya kila aina, pamoja na uwezo wake wa kucheza kama mshambuliaji wa kati au winga, unamfanya kuwa mchezaji muhimu kwa timu yoyote.
Mbio za Kusaini Wazir Jr. Zinazidi Kupamba Moto
Hata hivyo, Dodoma Jiji sio timu pekee ambayo ipo mawindoni kusaka saini ya Wazir Jr. Klabu nyingine kama Singida Big Stars na Pamba FC nazo zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyu mwenye kipaji kikubwa na uzoefu wa ligi kuu ya Tanzania. Lakini, inaonekana Dodoma Jiji wana nafasi kubwa zaidi ya kumsajili kutokana na historia yake na klabu hiyo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
- Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
- FIFA Yaiondolea Yanga Adhabu ya Kufungiwa Kusajili
- Dirisha la Usajili Ligi Kuu Tanzania kufunguliwa Juni 15 hadi Agosti 15, 2024
- Tetesi za Usajili Yanga: Okrah Kwenye Rada za Kuondoka Yanga? Habari Kamili
- Jinsi Ya Kuangalia Usajili Wa Namba ya Simu
- Tetesi za Usajili Real Madrid 2024/2025
Weka Komenti