TFF Kutangaza Washindi wa Tuzo za 2024/2025 Desemba 5 2025

TFF Kutangaza Washindi wa Tuzo za 2024/2025 Desemba 5 2025

Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) msimu wa 2024/2025 zinatarajiwa kutolewa Desemba 5, 2025 katika ukumbi wa The Super Dome jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imepangwa kukusanya wadau mbalimbali wa soka nchini, ikiwa ni sehemu ya kuwatambua wachezaji, makocha, marefa na timu zilizofanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya msimu uliopita.

Kwa mujibu wa maelezo ya TFF, tuzo zitakazotolewa zimegawanywa katika makundi makuu matano:

  1. Tuzo za Ligi Kuu ya NBC
  2. Tuzo za Kombe la Shirikisho la CRDB
  3. Tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake
  4. Tuzo za Ligi Nyingine
  5. Tuzo za Utawala

Aidha, msimu huu pia utashuhudia tuzo mpya kwa upande wa wanawake wanaocheza nje ya nchi, ikiwa ni mwendelezo wa tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania anayecheza nje ambayo ilianza kutolewa mwaka 2023/2024 kwa upande wa wanaume pekee.

TFF Kutangaza Washindi wa Tuzo za 2024/2025 Desemba 5 2025

Wachezaji Walioingia Kwenye Kinyang’anyiro cha Tuzo Kuu za Msimu

Katika upande wa Ligi Kuu ya NBC, mastaa watano kutoka Simba, Yanga na Azam wametajwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu. Wachezaji waliotangazwa na TFF ni:

  • Dickson Job (Yanga)
  • Pacome Zouzoua (Yanga)
  • Maxi Nzengeli (Yanga)
  • Jean Ahoua (Simba)
  • Feisal Salum (Azam FC)

Mmoja kati ya wachezaji hawa atavishwa taji hilo Desemba 5 pale Dar es Salaam, katika kilele cha hafla ya TFF Kutangaza Washindi wa Tuzo za 2024/2025 Desemba 5 2025.

Tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara

Sawia na upande wa wanaume, wachezaji watano wametajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake. Waliongia katika hatua ya mwisho ni:

  • Donisia Minja (JKT Queens)
  • Stumai Abdallah (JKT Queens)
  • Jeannine Mukandayisenga (Yanga Princess)
  • Jentrix Shikangwa (Simba Queens)
  • Esther Maseke (Bunda Queens)

Waamuzi na Makocha Wanaowania Tuzo

Katika kundi la waamuzi, TFF imetangaza majina matatu yanayowania Tuzo ya Refa Bora wa Ligi Kuu:

  • Ahmed Arajiga
  • Saad Mrope
  • Abdallah Mwinyimkuu

Kwa upande wa benchi la ufundi, makocha waliofanya vizuri msimu uliopita wamepenya kuwania Tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu:

  • Fadlu Davids (aliyekuwa Simba)
  • Rachid Taoussi (aliyekuwa Azam FC)
  • Ahmad Ally (JKT Tanzania)

Tuzo za Kombe la Shirikisho la CRDB

Katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, wachezaji watatu wameorodheshwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora:

  • Clement Mzize (Yanga)
  • Stephane Aziz Ki (Yanga)
  • Emmanuel Keyekeh (Singida Black Stars)

Tuzo za Wachezaji wa Tanzania Wanaocheza Nje ya Nchi

Kwa upande wa wachezaji wa kiume wanaocheza nje ya Tanzania, waliotajwa kuwania tuzo ni:

  • Mbwana Samatta
  • Novatus Dismas
  • Saimon Msuva

Kwa upande wa wanawake wanaocheza nje ya nchi, ambao watawania tuzo mpya iliyoanzishwa msimu huu, walioteuliwa ni:

  • Opa Clement
  • Diana Lucas
  • Enekia Kasonga

Katika taarifa yao, TFF imeeleza kuwa: “Msimu wa 2024/25 kutakuwa na tuzo moja mpya ambayo ni Mchezaji Bora wa Tanzania anayecheza nje upande wa wanawake.” TFF imekumbusha pia kuwa tuzo hii ilitambulishwa msimu wa 2023/24 lakini ilitolewa kwa upande wa wanaume pekee.

Zaidi ya Tuzo 40 Kushindaniwa

TFF imethibitisha kuwa zaidi ya tuzo 40 zitawaniwa katika hafla hiyo muhimu ya michezo nchini. Tukio hilo linatarajiwa kuwapa nafasi wadau kusherehekea mafanikio ya msimu, huku likitoa dira ya maendeleo ya soka la Tanzania kwa mwaka unaofuata.

Hafla ya TFF Kutangaza Washindi wa Tuzo za 2024/2025 Desemba 5 2025 inatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki na wadau kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo msimu uliopita katika ligi na mashindano mbalimbali.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba SC Yatambulisha Jezi Mpya Kwa Ajili ya Mechi za CAF 2025/2026
  2. Tuzo za CAF 2025 Kutolewa Leo Saa 3 Usiku Katika Hafla Kubwa Rabat Morocco
  3. Jezi Mpya za Yanga za Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2025/2026
  4. Kikosi cha Yanga Chawasili Zanzibar Kujiandaa na Mchezo wa AS FAR Rabat
  5. Kariakoo Dabi Yapigwa Kalenda Kutoka Desemba 13 Hadi Machi Mwakani
  6. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mikoa Yote (NECTA PSLE Results)
  7. Pantev Aandaa Mbinu Kali za kuizamisha Petro de Luanda Ligi ya Mabingwa Afrika
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo