Timu Yenye Makombe Mengi ya Ligi Kuu England (2024 ) | Hizi Ndio Timu Zilichochukua Kombe La Ligi Kuu England EPL Mara Nyingi Zaidi Kufikia Mwaka 2024.
Ligi Kuu ya Uingereza almaharufu kama ligi kuu ya EPL (England premier league) inasifika kama ndio ligi yenye mvuto zaidi duniani, hii ni kutokana na ushindani mkubwa uliopo kutokana na uwepo wa timu bora nyingi ambazo zinawachezaji wenye vipaji vikubwa kutoka maeneo mbalimbali Duniani. EPL imekua ndio ligi yenye matukio mengi ya kustajabisha kila msimu kutokana na aina ya ushindani ulipo ambapo mashabiki wa soka wamekua wakishuhudia matokeo yasiyo tabirika mara kwa mara.
Licha ya ushindani mkubwa uliopo katika Ligi kuu ya Uingereza, Zipo timu ambazo zimeweza kujiandika kwenye historia ya ligi hii baada ya kuchukua ubingwa maranyingi zaidi kuonesha ubabe haswa tangu enzi za miaka 90 hadi hii leo 2024. Vilabu kama Manchester United, Liverpool na Manchester City vimeonesha ubabe wake haswa katika michuano hii japo ya kuwa na ushindani mkubwa katika ligi.
Kwa kusema hayo, kwenye chapisho hili, tunaangazia vilabu ambavyo vimefanikiwa kushinda mataji mengi zaidi ya Ligi Kuu ya Uingereza tangu kuanzishwa kwake mnamo 1992.
Timu Yenye Makombe Mengi ya Ligi Kuu England (2024)
Manchester United ndio timu yenye makombe mengi ya ligi kuu England ambapo hadi msimu wa 2022/2023 imebeba ubingwa wa ligi kwa mara 13 tangu mwaka 1992.
Historia hii yakibabe ni ushahidi wa ubora wa klabu Manchester United ambayo kwa kiasi kikubwa ulitengenezwa na watu mashuhuri kama Sir Alex Ferguson. Ingawa Ubora wa Manchester united umepungua katika miaka ya hivi karibuni, Lakin bado klabu hii inasalia kuwa ndio klabu bora nchini Uingereza na yenye mashabiki wengi Duniani.
Misimu ambayo manchester united wameshinda ligi kuu ya Uingereza ni 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11 na 2012-13.
Hizi Ndio Timu Zilichochukua Kombe La Ligi Kuu England EPL Mara Nyingi Zaidi
Timu | makombe | Msimu |
Manchester United | 13 | 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13 |
Manchester City | 7 | 2011-12, 2013-14, 2017-18, 2018-19, 2020-21, 2021-22, 2022-23 |
Chelsea | 5 | 2004-05, 2005-06, 2009-10, 2014-15, 2016-17 |
Arsenal | 3 | 1997-98, 2001-02, 2003-04 |
Blackburn Rovers | 1 | 1994-95 |
Leicester City | 1 | 2015-16 |
Liverpool | 1 | 2019-20 |
Mapendekezo ya Mhariri:
- Orodha Ya Washindi Wa Ligi Kuu Ya Uingereza Miaka Yote
- Kylian Mbappé Atangaza Kuondoka PSG Huku Kukiwa na Tetesi za Kujiunga Real Madrid
- Makocha wanaowania Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka 2023/2024 Ligi Kuu ya Uingereza
- Orodha ya Wachezaji Wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana EPL 2023/2024
- Fainali Ya Klabu Bingwa Afrika 2024: Timu, Tarehe, Na Mahali
- Cheki Picha: Jezi Mpya za Liverpool kwa Msimu wa 2024/2025
- Fainali ya UEFA Champions League 2024: Real Madrid vs. Borussia Dortmund
Weka Komenti