Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026

Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026

Mechi za kuisaka tiketi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2026 zinaendelea kulindima katika mabara mbalimbali duniani, huku tayari baadhi ya mataifa yameshajihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano haya makubwa ya soka duniani. Hatua hii inazidi kuwasha moto wa ushindani kwa mataifa ambayo bado yanahangaika kutafuta nafasi zao kabla ya droo kubwa ya makundi itakayofanyika mwezi Desemba mwaka huu. Kombe la Dunia 2026 linatarajiwa kuwa la kipekee kwani litafanyika kwa mara ya kwanza kwenye nchi tatu kwa pamoja Marekani, Kanada na Mexico ambazo tayari zimejihakikishia tiketi ya kufuzu michuano hiyo kama wenyeji.

Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026

Mataifa Yaliyofuzu Kombe la Dunia 2026

Hadi sasa, mataifa yafuatayo tayari yameshajihakikishia kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2026:

Wenyeji

  1. Marekani
  2. Kanada
  3. Mexico

Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026 Bara la Asia (AFC)

  1. Australia
  2. Iran
  3. Japani
  4. Jordan
  5. Korea Kusini
  6. Uzbekistan

Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026 Bara la Afrika (CAF)

  1. Morocco (iliyoandika historia kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022)
  2. Tunisia

Bara la Amerika Kusini (CONMEBOL)

  1. Argentina
  2. Brazil
  3. Ecuador
  4. Uruguay
  5. Colombia
  6. Paraguay

Oceania (OFC)

  1. New Zealand

Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026 Bara la Ulaya (UEFA)

Bado michuano inaendelea na hakuna timu iliyothibitishwa kufuzu.

Timu Zilizobaki Kwenye Kinyang’anyiro cha Kufuzu

Mbali na timu zilizofuzu tayari, bado kuna nafasi nyingi zinazowaniwa. Katika bara la Afrika pekee, kuna nafasi saba zaidi zinazopiganiwa, huku bara la Ulaya likiwa na nafasi 16 zilizo wazi.

Asia (AFC): Qatar, UAE, Saudi Arabia, Indonesia, Iraq na Oman wanawania nafasi mbili za moja kwa moja pamoja na nafasi moja ya mchujo wa mabara.

Amerika ya Kusini (CONMEBOL): Bolivia tayari imefuzu kushiriki mchujo wa mabara baada ya kukosa nafasi sita za moja kwa moja.

Amerika ya Kaskazini, Kati na Caribbean (CONCACAF): Mataifa kama Honduras, Bermuda, Costa Rica, Trinidad & Tobago, Curacao, Haiti, Panama, Nicaragua, Jamaica, Guatemala, Suriname na El Salvador yameingia raundi ya tatu ya kufuzu. Kutoka hapo, timu tatu zitafuzu moja kwa moja huku nyingine zikishindania nafasi ya mchujo.

Oceania (OFC): New Caledonia imepata nafasi ya mchujo wa mabara.

Mataifa Makubwa Yaliyoondolewa

Michuano ya kufuzu pia imeleta mshangao baada ya mataifa makubwa kuondolewa mapema. Peru na Chile (waliomaliza nafasi ya tatu mwaka 1962) tayari wametupwa nje. Venezuela pia imeaga mashindano.

Kwa upande wa Asia, China ambao walitarajia kurejea Kombe la Dunia tangu waliposhiriki mara ya kwanza mwaka 2002, walikatishwa tamaa baada ya kutolewa Juni 5.

Kuelekea Kombe la Dunia 2026, tayari orodha ya timu zilizofuzu Kombe la Dunia 2026 inaanza kuchukua sura, huku mataifa makubwa kama Brazil, Argentina, Morocco na Japan yakihakikisha nafasi zao. Hata hivyo, bado kuna nafasi nyingi zinazopiganiwa na mataifa makubwa na madogo barani Afrika, Ulaya, Asia na Amerika. Mashabiki wa soka duniani wanasubiri kwa hamu kuona ni timu zipi zitakazojaza nafasi zilizobaki kabla ya droo ya makundi kufanyika Desemba mwaka huu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Azam FC Yawapa Mkono wa Kwaheri Wanne Kwa Mpigo
  2. Ratiba ya Ngao ya Jamii 2025/2026
  3. Kikosi cha Yanga 2025/2026 | Wachezaji Wote wa Yanga
  4. Kikosi cha Timu ya Taifa Wanawake U20 Kilichoitwa Kambini September 2025
  5. Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu ya NBC 2025/2026
  6. Ratiba ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026
  7. Ratiba ya NBC Premier league 2025/2026
  8. Simba yamtambulisha Wilson Nangu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo