Timu Zilizofuzu Robo Fainali AFCON 2025
Hatua ya Raundi ya 16 Bora ya Michuano ya AFCON 2025 imeanza kutimua vumbi rasmi, huku mataifa mbalimbali yakipambana kwa nguvu kubwa kutafuta nafasi ya kusonga mbele. Baada ya mechi zenye ushindani mkali na matukio ya kusisimua hadi dakika za mwisho, timu kadhaa zimefanikiwa kuipambania tiketi ya kuwafikisha katika hatua ya robo fainali ya michuano hii mikubwa barani Afrika.
Michuano ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) inatarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 9 na 10 Januari 2026, kabla ya hatua ya nusu fainali itakayofanyika tarehe 13 Januari. Mashindano yatahitimishwa kwa fainali kubwa itakayochezwa Rabat tarehe 18 Januari, ambapo bingwa wa AFCON 2025 atatajwa rasmi.
Orodha ya Timu Zilizofuzu Robo Fainali AFCON 2025
Mpaka sasa, timu mbili zimethibitisha nafasi yao katika hatua ya robo fainali ya AFCON 2025:
- Senegal
- Mali
Mali Yafuzu Kupitia Mikwaju ya Penalti Baada ya Vita Mkali Dhidi ya Tunisia
Timu ya taifa ya Mali imekuwa miongoni mwa timu zilizofuzu robo fainali AFCON 2025 baada ya ushindi uliopatikana kupitia mikwaju ya penalti. Mali ililazimika kucheza wakiwa na wachezaji 10 kwa sehemu kubwa ya mchezo, hali ambayo iliifanya mechi kuwa ya presha kubwa.
Mchezo huo ulipata bao la kwanza katika dakika ya 88 kupitia kwa Firas Chaouat. Hata hivyo, drama ilijitokeza mwishoni mwa mchezo baada ya Mali kupewa penalti ya dakika za majeruhi. Lassine Sinayoko alifanikiwa kuisawazisha mechi kwa bao la penalti katika dakika ya 97, na kuifanya matokeo kuwa 1-1.
Dakika za nyongeza hazikuzaa mabao, hivyo mshindi aliamuliwa kupitia mikwaju ya penalti. Bilal Touré alifunga penalti muhimu iliyoiwezesha Mali kusonga mbele na kufuzu rasmi robo fainali ya AFCON 2025.
Senegal Yapindua Meza na Kusonga Robo Fainali
Awali siku hiyo, Senegal nayo ilifanikiwa kufuzu robo fainali AFCON 2025 baada ya kuifunga Sudan kwa mabao 3-1. Licha ya Sudan kuanza kwa kishindo na kupata bao la mapema dakika ya sita kupitia Aamir Abdallah Yunis, Senegal iliweza kurejea mchezoni kwa kiwango cha juu.
Papa Gueye aliiongoza Senegal kwa kufunga mabao mawili kabla ya mapumziko, na kuipatia timu yake uongozi muhimu. Bao la tatu lilifungwa na Ibrahim Mbaye, na kuhakikisha Senegal inakata tiketi ya robo fainali kwa ushindi wa uhakika.
Kwa matokeo haya, Senegal sasa itakutana na Mali katika hatua ya robo fainali, mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia ya timu zote mbili na kiwango walichokionyesha kwenye Raundi ya 16 Bora.
Mapednekezo ya Mhariri:








Leave a Reply