Timu zilizofuzu Robo Fainali CHAN 2024
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeandika historia kwa kuwa ya kwanza kati ya timu zilizofuzu robo fainali CHAN 2024, baada ya kuibuka na ushindi wa tatu mfululizo katika hatua ya makundi. Ushindi huu ulipatikana kupitia mchezo wa kuvutia dhidi ya Madagascar, uliochezwa usiku wa Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa Kundi B, nyota wa Taifa Stars Clement Nzize alionyesha umahiri wa hali ya juu kwa kufunga mabao mawili ya haraka ndani ya dakika 20 za mwanzo. Madagascar walijibu mapigo kupitia mchezaji wao Nantenaina Razafimahatana, aliyepachika bao moja kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili kilishuhudia pande zote zikikosa nafasi kadhaa za wazi za kufunga. Hata hivyo, Tanzania ilidhibiti mchezo na kuhakikisha inalinda alama tatu muhimu, matokeo yaliyowapa tiketi ya kufuzu robo fainali wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Akizungumza baada ya mchezo, Mzize alisema:
“Ninafurahi sana kwa kufunga mabao mawili leo na kufuzu hatua ya robo fainali. Tunahitaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa sababu bado tuna mechi zaidi mbele yetu.”
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya CHAN tangu walipoanza kushiriki. Katika mashindano mawili yaliyopita, walishindwa kuvuka hatua ya makundi.
Orodha ya Timu zilizofuzu Robo Fainali CHAN 2024
- Tanzania (Taifa Stars)
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply